The House of Favourite Newspapers

NBC Kusaidia Wanafunzi Wanaoshindwa Kumudu Gharama za Ada Chuo Kikuu

0
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Emmanuel Mapunda (katikati) akisalimiana na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( DARUSO ) Bw. Hamis Mussa katika hafla ya kuchangisha fedha kwa njia ya vichekesho na burudani iitwayo  ‘Cheka Nisome’ iliyodhaminiwa na NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada. . Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC Bw. David Raymond.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa Benki ya  NBC Bw. David Raymond (kulia), akisalimiana na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( DARUSO ) Bw. Hamis Mussa katika hafla ya kuchangisha fedha kwa njia ya vichekesho na burudani iitwayo ‘Cheka Nisome’ iliyodhaminiwa na NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada. Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni Meneja wa NBC Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Emmanuel Mapunda.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond (kulia), akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika hafla ya kuchangisha fedha kwa njia ya vichekesho na burudani iitwayo ‘Cheka Nisome’ iliyodhaminiwa na NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada. Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Hafla hii iliratibiwa na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( DARUSO ).
Baadhi ya wahudhuriaji wakishangilia moja ya onesho lililokuwa likifanywa na mmoja wa wachekeshaji mahiri kutoka Kenya, Erick Omondi (hayupo pichani) katika hafla iliyoandaliwa mwishoni mwa juma lililopita na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( DARUSO ) na kudhaminiwa na Benki ya NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada chuoni hapo.

 

Leave A Reply