The House of Favourite Newspapers

Ndoa ya Maimartha yadaiwa kuvunjika

0

Maimartha Jesse ‘Mai’Maimartha Jesse ‘Mai’

Ubuyu: Hamida Hassan, Wikienda

DAR ES SALAAM: Ndoa ya mtangazaji maarufu wa Kipindi cha Muziki Mtamu cha Azam TV, Maimartha Jesse ‘Mai’ na mumewe, Raymond Shayo ‘Shaa’ inadaiwa kuvunjika na sasa mwanamama huyo anaishi kwa kujificha nyumbani kwa dada’ke maeneo ya Boko jijini Dar.

Ubuyu kutoka kwa sosi aliye karibu na mtangazaji huyo unadai kwamba, Mai aligombana na mumewe huyo kwa sababu ya kupenda kwenda kwenye shughuli kila kukicha na kuacha majukumu ya kifamilia, ndiyo maana akatimuliwa na kwenda kukaa kwa dada’ke, Boko.

MAIMARTHA2APONZWA NA SHEREHE ZA KILA SIKU

“Hivi Wikienda mna ubuyu kuwa Maimartha hayupo nyumbani kwake Kisemvule (Mkuranga, Pwani?)

“Kwa taarifa yenu amekorofishana ile mbaya na mumewe. Unajua mumewe hapendi mambo ya shughuli (sherehe) za kila siku.

“Si mnajua Mai ni MC (Master of Ceremonies)? Sasa mumewe kuna wakati huwa anamkatalia kwenda kwenye hizo shughuli lakini Mai huwa hasikii.

“Wiki mbili zilizopita inasemekana Mai alilazimisha kwenda kwa sababu alikuwa ameshapokea mkwanja wa watu hivyo akaondoka kinguvu, aliporudi mumewe akamtimua,” alinyetisha sosi huyo kwa sharti la kutochorwa gazetini.

NYUMBANI KWA DADA WA MAI

Baada ya ishu hiyo kutua kwenye meza ya Wikienda, mwanahabari wetu alimfuata

 Mai nyumbani kwa dada’ke Boko ambapo aliambiwa kuwa Mai hakuwepo anaishi nyumbani kwake, Kisemvule.

Mwandishi wetu alifunga safari hadi nyumbani kwa Mai huko Kisemvule ambapo aliambiwa kuwa mwanamama huyo amesafiri.

MAI AFUNGUKA

Mai mwenyewe alipotafutwa kwa njia ya simu na kusomewa mashtaka yake, kwanza alitoa lugha mbaya kisha akafunguka machache katika mahojiano na Wikienda.

Wikienda: Mai mambo vipi? Uko wapi kwa sasa?

Mai: Nipo nyumbani kwangu, Kisemvule

 nimepumzika baada ya kutoka kwenye kipindi changu si unajua tena!

Wikienda: Mbona nimekuja nyumbani kwako nimeambiwa umesafiri, ina maana nikija hata muda huu nitakukuta?

Mai: Ulikuja lini? Mbona unakuja kwangu bila taarifa? Kama namba yangu unayo inakuwaje sasa unanivamia hivyo? Mimi nipo kwani una shida gani?

Wikienda: Nasikia ndoa yako imevunjika au umeachika kwa Shaa kwa sababu ya shughuli na sasa unaishi kwa dada’ko, Boko. Je, ni kweli?

Mai: Mh…! Wewe unanitafuta, sasa nikwambie tu mimi na mume wangu hatuwezi kuachana, ndiyo kwanza penzi limeanza upya na aliyekuambia amekosea njia.

Wikienda: Hakuna aliyewahi kukubali kuwa ameachwa, wewe funguka, mbona nilikuja kwako nikaambiwa umesafiri na wewe unaniambia upo? Funguka kwa sababu dunia haina siri.

Mai: Mimi mara nyingi sionekani nyumbani kwa sababu nakuwa kwenye maandalizi ya kipindi changu cha Muziki Mtamu. Kwa sasa naandaa season (msimu) ya pili sasa kunikuta tu nyumbani siyo rahisi.

Mai na Shaa walifunga ndoa Februari Mosi, mwaka 2012 ambapo wamejaliwa mtoto mmoja.

Leave A Reply