The House of Favourite Newspapers

Nguvu ya Global Group & V.O.A Yazidi Kuimarika Kimataifa

0
Mkurugenzi wa Masoko Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika wa V.o.A, Joyce Ngoh (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo (kulia) na Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.

 

MKURUGENZI  wa Masoko Joyce Ngoh, Mashariki na Kusini mwa Afrika kutoka wa Shirika la Habari la Amerika, Voice of America (V.o.A) yenye makao yake makuu Washington D.C, Marekani amefanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makampuni ya Global Group zilizopo Sinza, jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi, Disemba 5, 2019.

Wakiwa ndani ya studio za Global TV Online.

 

Akizungumzia Ujio huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group Eric Shigongo amepongeza shirika hilo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuuhabarisha umma katika mabara yote ya dunia na kuwataka waendeleze ushirikiano uliotukuka na Global Group kwa manufaa ya watu wote.

Bi Joyce akifurahia jambo na mtangazaji wa Kipindi cha Bongo 255 cha Globa Radio, Judith daffa ‘Juju’.

Shigongo amesema anajivunia ushirikiano huo huku akiahidi kushikamana na VoA kwa kubadilishana habari, kutoa habari zenye weledi na tija kwa umma na taifa zima na kuongeza kuwa Global TV Online ambayo ni Televisheni inayoongoza kwa ubora na kufuatiliwa na watu wengi zaidi nchini, itaendelea kutoa habari zilizo bora kwa kuzingatia sheria za nchi, maadili na kanuni za tasnia ya habari.

 

Kutoka kushoto ni Meneja wa vipindi wa Global Radio, Borry Mbarakah, Bi. Joyce, Abdallah Mrishio na Minyingi Japhet ambaye ni Ofisa Huduma ya Masoko Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika wa V.o.A.

 

Mbali na kukuza ushirikiano huo, Mkurugenzi huyo wa V.o.A, alifika pia kwa ajili ya kujifunza namna ambavyo Global TV na Global Radio wamekuwa wakifanya kazi zao za uandishi kwa weledi jambo lionalowavutia watazamaji na wasikilizaji wao duniani kote.

Wakiteta jambo ndani ya Studio za Global Radio.

 

Kwa sasa Global TV Online na mtandao wa www.globalpublishers.co.tz vimekuwa vikishirikiana na VoA kwa miaka mingi ikiwa ni pamoja na habari, matukio, picha na video zinazopatika kwenye mitandao hiyo ambazo zimekuwa zikitumiwa na VoA, na habari zinazorushwa na VoA zimekuwa zikitumiwa pia na Global TV Online na www.globalpublishers.co.tz.

Bi Joyce akiwa na watangazaji wa kipindi cha MidMorning Fresh ndani ya studio za Global radio.

Pia kuna vipindi na taarifa za habari (Duniani Leo, kila siku jioni) kutoka VoA ambavyo vimekuwa vikirushwa kupitia Global TV Online ikiwemo;

Washington Bureau, kinachotangazwa na Sunday Shomari kila Jumanne saa 5:00 asubuhi, Shaka Extra Time cha Shaka Ssali kila Jumatano saa 5:00 asubuhi na Straight Talk of Africa cha Shaka Ssali, kila Alhamisi saa 5:00 asubuhi.

 

 

Akisaini katika kitabu cha wageni katika ofisi za Global Group.

 

Bi Joyce akizungumza jambo na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally.

 

Leave A Reply