The House of Favourite Newspapers

Nilifanya Mapenzi na Maiti 20 Nitajirike – 10

maiti-cover

ILIPOISHIA SEHEMU YA TISA

“Huu una masharti makubwa mawili,” aliniambia mganga.

“Yapi?”

“Moja, unatakiwa kuwaua wazazi wako wote wawili,” aliniambia huku akikishika kitunguli kidogo kilichokuwa pembeni yake.

“Kuwaua wazazi wangu?”

“Ndiyo!”

“Na sharti jingine?” niliuliza huku nikionekana kuchanganyikiwa.”

“Kufanya mapenzi na maiti ishirini..” aliniambia.

MWAGIKA NAYO HAPA…

Kwanza nikashtuka, sikuonekana kuamini kile alichoniambia, nikamuuliza mara mbilimbi alisemaje, yeye akaniambia vilevile kwamba nilitakiwa kufanya mapenzi na maiti ishirini kama nilitaka kuwa tajiri, hivyo nilitakiwa kuchagua.

“Umechagua nini?”

“Kati ya nini na nini?”

“Kuwaua wazazi wako au kufanya mapenzi na maiti ishirini?” alinijibu kwa kuniuliza swali.

“Bora nifanye mapenzi na maiti ishirini…” nilimwambia japokuwa niliogopa mno.

Alichokifanya mzee yule ni kuchukua unga mwingine na kunipaka usoni kisha kuniambia nitulie kwa muda. Nilitulia hapohapo, sijui nini kilitokea, ghafla, nikajikuta nikitokea katika hospitali moja kubwa hapa jijini Dar es Salaam, nilishangaa, nilijiuliza nilifikikaje mahali hapo lakini sikuwa na jibu lolote lile.

Kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakiendelea na shughuli zao, wagonjwa waliokuwa wakiingia na kutoka. Ghafla, nikasikia sauti ya yule mzee ikiniambia kwamba nilitakiwa kwenda mochwari, sikujua ilikuwa wapi lakini nikajikuta nikijiongoza mpaka kufika katika mlango ambao uliandikwa MOCHWARI kwa nje.

“Subiri hapo mpaka usiku,” niliisikia sauti hiyo.

Nilifanya kama nilivyoambiwa, nikasubiri mahali hapo. Ilikuwa jioni kama saa kumi na moja hivi. Hakukuwa na mtu aliyeniona, wengi walinipita bila kunisalimia. Ilipofika saa moja usiku, nikasikia sauti ile ikiniambia niende ndani ya mochwari ile, maelekezo mengine angeniambia, nikafanya hivyo na kuanza kuingia humo ambapo kulikuwa na masanduku mengi yaliyokuwa na maiti nyingi. Nikaambiwa nisubiri. Nakuja kutahamaki, eti ilikuwa saa sita usiku. Nikabaki nikitetemeka tu.

*****

Ulikuwa usiku mkubwa, nakiri kwamba hakukuwa na sehemu iliyokuwa inatisha kama ilivyokuwa mochwari. Ndani ya mochwari ile, kulikuwa na majeneza ya maiti ambazo zililetwa humo ndani na nyingine tayari kwa kuchukuliwa lakini pia kulikuwa na masanduku mengi ambayo ndani yake kulikuwa na maiti, baridi lililokuwa humo ndani, lilikuwa kubwa mno.

Humo kulikuwa na walinzi wawili, walikuwa wakilinda, nilijiuliza walipata wapi ujasiri wa kuwa ndani ya chumba kile, tena usiku mzima huku wakionekana kutokuwa na hofu hata kidogo.

Mimi, sikuwa nikionekana, yaani hata niliposogea karibu yao, hawakuwa wakiniona zaidi ya kufanya vitu vyangu. Humo, ndipo nilipojifunza kwamba kulikuwa na mambo mengi yaliyokuwa yakitokea.

Niliwaona watu wakija usiku huohuo, walikuwa wakizungumza na walinzi hao na kuwaambia shida zao, wengine walifika kwa kuwa walihitaji baadhi ya viungo kutoka kwa maiti ili waende kufanya mambo yao ya kishirikina.

Nilimuona mlinzi mmoja akitoka na kwenda kwenye sanduku moja, akalivuta kisha kuanza kuitoa maiti iliyokuwa humo ndani. Mwili wangu ulisisimka mno, sikuamini nilichokuwa nikikiona, hofu ilinijaa moyoni mwangu.

Mlinzi yule akaivua nguo maiti ile, sikujua alichokuwa akikihitaji, yale mambo ambayo nilikuwa nikiyasoma kwenye vitabu vya kusisimua, siku hiyo nilikuwa nikiyaona kwa macho yangu.

Akachukua kisu ambacho alikihifadhi sehemu maalumu, nyuma ya mlango na kisha kuanza kukata kifundo cha mguu cha maiti ile kwani ndicho kilichokuwa kikihitajika kwa hali na mali.

Ninayoyazungumza hapa, niliyashuhudia kwa macho yangu. Mapigo yangu ya moyo yalikuwa juu mno, japokuwa kile kilikuwa kikifanywa kwa maiti lakini niliogopa na kuionea huruma, niliona kama ilikuwa ikionewa.

Alipomaliza, mlinzi akakichukua kifundo cha mguu ule na kisha kumpa mwanaume aliyekuwa amekifuata na kuondoka nacho. Walinzi waligongesheana mikono, kila mmoja alionekana kuwa na furaha.

Wala haukupita muda mrefu, nikaona mlinzi mmoja akitoka nje. Sikutaka kubaki ndani, wakati namsubiria yule mganga, nilitaka kujua ni kitu gani kingine kilichokuwa kikitokea.

Nilimfuata mlinzi, alikwenda moja kwa moja kwenye gari moja ya kifahari, Range SUV nyeusi na kuongea na mtu aliyekuwa humo ndani. Nilisogea kwani nilitaka kuyasikiliza mazungumzo yao.

“Nahitaji maji ya maiti,” alisema mzee aliyekuwa humo ndani ya gari.

“Laki mbili! Hela ipo?” aliuliza mlinzi yule.

“Ipo! Naomba ukaniwekee humu!”

Yule mzee sikuweza kumfahamu kwa kipindi kile lakini sauti yake, hapo baadaye nilimfahamu kwani nilikutana naye mara kwa mara. Baada ya kuzungumza hivyo, akatoa kidumu na kumpa mlinzi yule ambaye akakichukua na kuondoka nacho.

Sikutaka kubaki hapo nje, nikamfuata mlinzi mule mochwari alipokwenda. Nilipoingia, nikakuta akimwambia mwenzake kwamba kulikuwa na dili jingine, kuna mtu alifuata maji ya maiti.

“Hakuna tatizo! Twende kule kwenye maiti za wiki iliyopita!” alisema mlinzi aliyeletewa taarifa.

****

Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia kesho hapa kujua kitakachoendelea katika sehemu ya 11

MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI

halotel-strip-1

Comments are closed.