The House of Favourite Newspapers

Nilifanya Mapenzi na Maiti 20 Nitajirike – 4

maiti-cover

ILIPOISHIA SEHEMU YA TATU

“Kwa hiyo hauna ndugu?” aliniuliza.

“Ndiyo! Ila nakwenda kutafuta maisha…” nilimjibu.

Akanionea huruma, kiukweli macho yake yalionyesha jinsi gani hakutaka mimi niende huko lakini hayakunishawishi niendelee kubaki hapo Ifakara, iwe isiwe ilikuwa ni lazima niendelee na safari ya kuelekea Dar es Salaam, kama wazazi walishindwa kunizuia, basi niliamini hata huyo Mudi naye asingeweza.

“Una nauli sasa?” aliniuliza.

MWAGIKA NAYO HAPA….

Alichokifanya ni kunipokea begi langu na kunipeleka ndani ya daladala lile. Nilikaa huku nikiwa najifikiria ni kitu gani kingetokea mara baada ya kufika Ifakara. Nilipomwangalia utingo ambaye nilimsikia dereva akimuita kwa jina la Mudi, muda wote alionekana kuwa mwenye furaha tele, abiria walipojaa ndani ya gari, dereva akaliwasha na kuanza safari ya kuelekea huko.

Utingo huyo alikuwa akifikiria ngono, ila kichwa changu kilikuwa kikifikiria utajiri tu ambao niliamini kwamba ningeweza kuupata baada ya kufika jijini Dar es Salaam.

Bado akili yangu ilikuwa ikimfikiriaMudi, alionekana kuwa mwenye furaha tele kwani alijua kwamba siku hiyo mambo yake yangekwenda vizuri kabisa. Nilikuwa na hofu, nilichokuwa nikikifikiria ni namna ya kumkimbia mara baada ya kufika Ifakara.

Safari iliendelea, hakukuwa na abiria aliyekuwa akizungumza kitu chochote kile, kila mmoja alikuwa kimya. Daladala iliendelea kwenda mpaka tulipokaribia Ifakara ambapo huko abiria wangeshuka na kuchukua mabasi makubwa kwa ajili ya kuvuka ya kuelekea Ruaha kisha kuvuka Mbuga ya Mikumi na hatimaye kuingia Morogoro Mjini.

Kutoka hapo kijijini Lupiro mpaka Ifakara tulitumia saa tatu njiani. Barabara haikuwa nzuri hata mara moja, ilikuwa mbaya iliyokuwa na mashimoshimo mengi. Mara baada ya kuingia Ifakara moja kwa moja nikateremka kutoka ndani ya gari huku tayari ikiwa ni saa mbili asubuhi.

Muda wote Mudi alikuwa akiniangalia kwa macho ya matamanio, alionyesha ni jinsi gani alikuwa na uchu na mimi. Sikutaka kujali sana, sikutaka kumtoroka japokuwa nilikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Kumbuka kwamba sikuwa na fedha, nilikuwa na begi langu tu lakini nia yangu ilikuwa ileile ya kutaka kuingia ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mambo yangu na nipate fedha.

Wakati nikiwa nimekwenda pembeni na kujiinamia, akanisogelea na kuniambia niende nyumbani kwake ambapo wala hakukuwa mbali kutoka mahali hapo. Sikukataa, nilikubaliana naye na kuanza kuelekea huko. Njiani alinishika mkono kama mke wake, kwa kumwangalia, alikuwa mtu wa sifa, alitaka kuonekana kwamba alikuwa na msichana mrembo, mwenye mvuto kwani kwa umbo langu hasa nyuma, nilikuwa nimejazia sana.

“Hapa nimewaweza…” aliniambia huku akiachia tabasamu pana.

“Wakina nani?”
“Hawa watu, wanafikiri kwamba sisi wengine hatuna uwezo…” aliniambia.

“Uwezo gani?”

Hakutaka kunijibu swali hilo, akalipotezea kwa kuingiza stori nyingine kabisa, nilijua alichomaanisha ila sikutaka kujali, nilichokifanya ni kubaki kimya na kuelekea nyumbani kwake.

Baada ya muda fulani tukaingia katika nyumba moja iliyokuwa kuu-kuu, nje kulikuwa na kibaraza kilichoharibika, ukuta ulikuwa na rangi iliyopauka, mabati yake yalikuwa na kutu, kwa jinsi ilivyoonekana, ilionyesha kwamba mwenye nyumba hiyo hakuwa akiijali, inawezekana hakuwa na fedha za kuikarabati au aliiacha kwa makusudi yake.

Tukapiga hatua kwenye korido ambapo kulikuwa na wanawake wawili waliokuwa wakizongea mambo yao, walipomuona Mudi akiingia nami, niliona kabisa wakishtuka ila wakazuga kama hawakushtuka kitu chochote kile, wakaanza kuzungumza naye kwa utani mwingi.

“Naona leo umetuletea shemeji…” alisema mwanamke mmoja.

“Hahah! Ndugu yangu bwana…” alijibu huku akicheka.

“Eti ndugu yako! Undugu gani huo mpaka chumbani,” alisema mwanamke mwingine, Mudi hakutaka kuongea kitu kingine, akaongeza tabasamu na kisha kuingia naye chumbani.

Chumba chake hakikuwa kizuri sana, kilikuwa moja ya chumba kilichomilikiwa na mtu asiyekuwa na pesa kama nilivyokuwa. Kulikuwa na kitanda kidogo, godoro lililochakaa, ndani humo kulikuwa na vyombo ambavyo havikuwekwa katika mpangilio maalumu, yaani kwa kifupi hakikuwa kizuri.

“Karibu sana mrembo…” aliniambia huku akichgia tabasamu.

Kwa mara ya kwanza nikalala na Mudi, sikupenda kufanya hivyo lakini kiukweli sikuwa na jinsi. Sikuwa nikiifahamu historia yake kimapenzi, sikujua alikuwa na nani kabla yangu lakini kutokana na uhitaji niliokuwa nao, sikuwa na jinsi, kwa usiku huo alinifanya kuwa mke wake.

Asubuhi ilipofika, nilimwambia kwamba ningeondoka, japokuwa alining’ang’ania sana nibaki lakini nilikataa, nilimweleza wazi kwamba nilikuwa na safari ya kuelekea jijinii Dar es Salaam, sehemu ambayo sikuwa na ndugu hata mmoja.

“Kwa hiyo hauna ndugu?” aliniuliza.

“Ndiyo! Ila nakwenda kutafuta maisha…” nilimjibu.

Akanionea huruma, kiukweli macho yake yalionyesha jinsi gani hakutaka mimi niende huko lakini hayakunishawishi niendelee kubaki hapo Ifakara, iwe isiwe ilikuwa ni lazima niendelee na safari ya kuelekea Dar es Salaam, kama wazazi walishindwa kunizuia, basi niliamini hata huyo Mudi naye asingeweza.

“Una nauli sasa?” aliniuliza.

Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia kesho hapa kujua kitakachoendelea katika sehemu ya tano.

MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI

halotel-1

Comments are closed.