The House of Favourite Newspapers

Niliongea na Mwanangu Saa Chache Kabla ya Kifo Chake – Baba Mzazi wa Ismail

kifo-cha-ismail-2

BABA mzazi wa marehemu Ismail Mrisho Khalfan aliyefariki jana akiwa uwanjani, Khalfan Mrisho   aishiye jijini Mwanza amesema kwa mara ya mwisho aliongea na mwanaye jana asubuhi na mchana saa chache kabla ya mchezo wa Mbao FC na Mwadui FC.

“Mwanangu aliniambia ana furaha sana na anaomba nimuombee dua katika michuano ya U-20 ili waweze kufuzu na baadaye mipango yake ya kwenda nje ya nchi iweze kukamilika.” Alisema Mzee Khalfan Mrisho kwa masikitiko.

Mshambuliaji Ismail Mrisho Khalfan amefariki dunia jana jioni baada ya kuanguka uwanjani Kaitaba, Bukoba wakati wa mtanange wao dhidi ya timu yake ya vijana wa Mbao FC ya mkoani Mwanza dhidi ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga, ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la Ligi ya Vijana.

kifo-cha-ismail-1

Naye Mwakilishi wa Kituo cha Football House alicholelewa marehemu Ismail, Francis Felician naye alikuwa na haya ya kusema;

“Tumepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Ismail, tumekuwa naye kwa zaidi ya miaka mitano na ni mmoja wa vijana tulioanza nao na tayari alikuwa amepata dira ya kutoka kisoka maana alikuwa tayari alikuwa na scholarship ya kwenda chuoni nchini Marekani

“Mwezi Juni alikwenda Marekani kwa majaribio ya wiki mbili na alikuwa amefaulu kufadhiliwa kwenda nchini humo na alikuwa anasuburi kumaliza mitihani wa kidato cha nne aliyomaliza hivi karibuni ili aondoke.”

halotel-strip-1-1

Comments are closed.