The House of Favourite Newspapers

Nisha: Watoto Yatima Ndiyo Starehe Yangu

0

nisha (4) Salma Jabu ‘Nisha’ akila chakula cha pamoja na watoto yatima.

STAA anayetamba na filamu ya Kiboko Kabisa, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema wakati nyota wenzake wanapenda starehe za dunia yeye furaha yake kubwa ni kuona watoto yatima wanapata mahitaji yao muda muafaka.

nisha (1)“Naguswa sana na watoto hawa, hivyo kila mwisho wa mwezi huwa nakuja kuwatembelea na kuwasaidia baadhi ya changamoto walizonazo, leo nimewahi kwa sababu sitakuwepo mwisho wa mwezi maana nitasafiri nje ya nchi, hii ndiyo starehe yangu, maana huwa wananiombea dua mambo yananinyookea kila siku,” alisema Nisha.

Nisha alitoa kauli hiyo alipowatembelea watoto yatima wa Kituo cha New Hope Group kilichopo Kigamboni, Dar hivi karibuni.

 

Leave A Reply