BENKI ya NMB imekabidhi zawadi kwa washindi tisa wa MastaBoda kama washindi wa wiki baada ya kufikisha
miamala hamsini kupitia mfumo wa malipo wa Mastercard QR katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Zoezi hilo liliendeshwa na Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi- Yusuph Achayo na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa
Waendesha Bodaboda- Michael Massawe.
MastaBoda ni kampeni inayoendeshwa na NMB kwa ajili ya kuwawezesha waendesha Bodaboda kuunganishwa
katika mfumo wa kibenki ili waweze kupokea malipo kupitia mfumo wa Mastercard QR pamoja na mitandao ya
simu iliyo unganishwa na mfumo wa malipo wa Mastercard QR.
Akikabidhi zawadi hizo Achayo ametoa wito kwa waendesha Bodaboda ambao hawajajiunga na mfumo wa
MastaBoda kujiunga ili kuendesha biashara zao kisasa kwa usalama wa fedha zao.
Nao washindi walioibuka na kitita cha Sh, 50,000. Wameimwagia sifa NMB kwa kutimiza ahadi, kwani
zinawaongezea nguvu ya kupambana ili kufika mbali zaidi katika kuendesha biashara zao.
“Tangia nijiunge na mfumo huu, hii ni mara yangu ya pili kushinda, najisikia furaha sana. Tangu nianze kufanya
miamala na QR nina amani, badala ya kutembea na pesa sasa fedha yangu inaingia moja kwa moja benki, mfumo
huu pia unaookoa muda hasa katika kutafuta chenchi. .”alisema Ebenezer Elisha (Mwenge) ambaye pia ni mmoja
wa washindi.
Washindi wengine waliojizolea kitita hicho ni Goodluck Ntaya (Kawe Ukwamani), Mohamed Abdallah (Buguruni
Rozana) Twaliha Mfinanga(Rozani Mafleti) na Frorian Byabato (Roziani Mafleti).