The House of Favourite Newspapers

NMB Yapongezwa na Waziri wa Fedha na Mipango

nmb-1

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango anayekata utepe (katikati) na kulia kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ambapo kushoto kwake ni Mkuu wa Kitengo Cha Biashara wa NMB, James Metairon.

nmb-2

Baadhi ya wafanyakazi wa NMB waliofika kwenye maonyesho hayo wakitoa ufafanuzi wa jambo kwa Waziri Mwinjage (kushoto) na Waziri Dk.Mpango.

nmb-3

..Dk.Mpango akisoma hotuba yake katika hafla hiyo.

nmb-4

Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage akizungumza jambo katika hafla hiyo.

nmb-5

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB, James Metairon naye akizungumza jambo.

nmb-6

Ofisa wa Kitengo cha Uongozaji wa Imori International, Matrina Ambrozy akieleza jambo katika hafla hiyo.

nmb-7

Mkurugenzi wa Imori International, Leo Mukirya (kushoto) akimtembeza Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Patrick Nkandi (kulia).

nmb-8

Baadhi ya bidhaa iliyopo kwenye maonyesho hayo.

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango, leo ameipongeza benki ya NMB kwa juhudi zake inazozionesha katika utoaji wa mikopo na riba nafuu kwa wajasiliamali wadogo.
Hayo ameyasema leo katika ufunguzi wa maonyesho ya sekta ya kibenki na fedha yaliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Dk. Mpango amewapongeza waandaaji wa maonyesho hayo ambao ni Imori International kwa kuona umuhimu wa kuanzisha utaratibu wa maonyesha katika sekta ya fedha katika maendeleo ya viwanda na uchumi kwa taifa ambapo ndio yameanza kwa mwaka huu.
Amesema, serikali kwa kupitia wizara ya fedha na mipango, wizara ya viwanda na biashara inawahakikishia kuwapa ushirikiano katika kuendeleza utaratibu mzuri.

“Kwanza napenda nitoe pongezi kwa benki ya NMB PLC (National Microfinance Bank Plc) kwa kuona umuhimu wa kudhamini maonyesho haya kwani udhamini huu umetupatia wote fursa ya kukutana na kuonyesha jamii huduma zinazotolewa na sekta ya fedha na shughuli za wajasiliamali ambao wana kiu kubwa ya mitaji ili kwa pamoja tushirikiane kujenga Tanzania ya viwanda,” alisema.

Akaongeza: “Serikali inatambua mahitaji makubwa ya kufanya maboresho na kuwezesha mabenki na taasisi nyingine za kifedha kuweza kufikia watu wengi kwa maana ya mitaji ya kutosha ya kuongeza uwekezaji wa ndani.
“Serikali imedhamiria kuweka msukumo zaidi kujenga mazingira rafiki kwa wadau wa sekta hi ili iweze kupanua huduma zake hapa nchini na hivyo kuchochea uzalishaji na upatikanaji wa huduma bora za jamii,” Aidha amewataka waandaaji kufanya maonyesho hayo katika mikoa mingine ili hata kule ambapo taasisi hizi za kifedha na benki ni chache, basi zipate hamasa kuwekeza huko kama chachu ya maendeleo ya taifa.

Alitoa msisitizo kuwa mbali na mabenki hayo kufanya biashara, hivyo ni wajibu kwa wajasiliamali nao kwenda wakiwa na miradi mizuri inayokopesheka na wakipata mitaji basi waitumie ilivyokusudiwa na waweze kurudisha kwa wakati muafaka.
Kauli mbiu ya maonyesho hayo ilikuwa ni “Fursa Katika Dunia ya Kifedha”.

Na Denis Mtima/Gpl

Comments are closed.