The House of Favourite Newspapers

Nyalandu Atusua Uchaguzi Chadema

0

ALIYEKUWA Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameshinda nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Kati kwa kupata kura 60 kati ya 86 zilizopigwa na kumshinda aliyekuwa mwenyekiti wa kanda hiyo, Alphonce Mbasa.

 

Akitangaza matokeo hayo jana Jumapili Desemba 1, 2019, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrick Sosopi akisaidiana na katibu mkuu wa baraza hilo, Julius Mwita. amesema waliopiga kura walikuwa 86, hakuna kura iliyoharibika.

 

Amesema aliyekuwa mwenyekiti wa Kanda hiyo, Alphonce Mbasa amepata kura 26, sawa na asilimia 33.2.

 

Katika nafasi ya mweka hazina, Mbunge wa Viti Maalum, Devotha Minja ameibuka mshindi baada ya kupata kura 44 sawa na asilimia 51.2 huku mshindani wake, Tully Kiwanga akipata kura 42 sawa na asilimia 48.8.

Leave A Reply