Okwi Afungua Akaunti Ya Mabao Misri

KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Simba hivi sasa anayekipiga Al Ittihad Alexandria ya Misri, Mganda Emmanuel Okwi, amefungua akaunti ya mabao kwa kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 3-0.

 

Ittihad ilipata ushindi huo katika mchezo wa Ligi Kuu ya nchini huko ilipocheza na Ismaily, mchezo uliokuwa na ushindi mkubwa kwa timu zote hizo.

 

Hilo ni bao lake la kwanza kulifunga mshambuliaji huyo tangu ajiunge na timu hiyo kwenye msimu huu wa ligi akitokea Simba baada ya kumaliza mkataba wake wa kuitumikia timu hiyo.

 

Okwi mwenye sifa ya kukokota mpira huku akipiga chenga za maudhi, alifunga bao hilo katika dakika ya 42 ya mchezo huo huku akifanikiwa kuibuka mchezaji bora wa mchezo huo.

 

Mabao mengine ya Ittihad yalifungwa na Rizk katika dakika ya 21 huku lingine likipachikwa na Cisse dakika ya 51.


Loading...

Toa comment