The House of Favourite Newspapers

Oya masela kama vipi bora mkoa… Bongo lazima utumie ubongo

0

Niaje niaje cha-ma langu la ukwehe? Inakuwa nini sasa kitaa hiyo? Kipande hii ni mpango mzima, kitu kanyaga twende bati masti utumie maakili siyo kwenda-kwenda tu bila madaireksheni. Welikamu kwa sana kwa fasi ya jamvini tukinukishe wazazi ama nene? Basi barida!

Wanangu siyo sekreti lasti wikiendi kuna mwanangu mmoko alinitoa na listori la mai waifu wake ambaye alitaka kujitoa kitu cha pumzi mwenyewe aisee arifu.

Msela amekuwa na mbebiz wake mkare kwa miaka bee sasa. Miezi f’lani iliyokrosi mai waifu wa mshkaji alikuwa mbali kiduchu na jamaa yangu bati komyunikesheni ilikuwa kama dawizi kama kawizi. Yaani chitchati za deile za kufa mtu. Si unanyaka tena mitikasi ya mawasapu?

Kachala anakuteli kwamba waifu wake ni fulu kwere! Yaani ana mawivu hatare. Ilikuwa kwikwi kozi mtoto mzuri pale kati alipitiliza so akaamua kupiga dauni kibarua kisha kumuibukia msela kitu cha mkoani ili akatumikie lavu. Wana wanakuteli kuwa kama vepe bora mkoani kuliko Bongo tambarare ambapo kichwa masti kitumie ubongo ili kusavaivu. Sasa utachezaje mbali na ubavu wako?

Ilikuwa jioni moko hivi, selaa akiwa jobu alivutiwa waya na kichwa mmoko anayegonga naye jobu, akamteli kuwa ana mgeni. Mwana hakubilivu kozi mai waifu wake ilikuwa ni ngumu kinoma kumtimbia bila infomesheni bati kwa kuwa shori wake zinagongagonga, akahisi tu atakuwa yeye mama la mama.

Kweli kaka mkubwa alipojisogeza tu akampiga chabo mbebiz wake mkaree. Jamaa yangu alichokifanya ni kumpokelea makago nini na nini kisha akammuvuzisha skani. Katika situwesheni isiyosomeka freshi, njiani shori alikuwa hapigi mastori kama anavyokuwa nomo.

Walipotimba kwa mahomu sasa, waifu wa mshkaji alizunguka na kupekuwa hausi nzima. Si unajua zile? Alikuwa anahisi atakuta evidensi yoyote kama jamaa alikuwa anaingiza mpango wa kando. Shori alipomisi alichokuwa akikitafuta si ndo akaanza kutupia swaga za maneno makali aibu?

Baada ya kuona msela hataki kuikuza ishu kwa kunyuti, shori aliendelea kumtisha jamaa kwamba yupo rede kukisanua hata kwa majirani ili tu kumchafua.

Shori alipoona jamaa anazidi kumpotezea alizunguka nyuma ya hausi dheni akagonga kitu cha sumu. Saluti iende kwa jirani mmoko aliyeokoa jahazi na kumkimbiza hospito kisha kusevu laifu lake.

Ebana wanangu mmenisoma? Ungekuwa ni wewe selaa ungefanyaje? Kaa humu wewe upate maujanja.

Sii yuu neksi wiki
mzazi jembe!

Leave A Reply