The House of Favourite Newspapers

Papa Francis awasili Kenya

0

PAPA (7)Kiongozi wa Wakatoliki duniani, Papa Francis wa Kwanza akiwasili leo Kenya.

PAPA (1)

Akiwasiliana na kiongozi wa Wakatoliki nchini Kenya.

PAPA (9)

Papa Francis akisalimiana na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Maneno aliyoandika Baba mtakatifu Francis baada ya  kuwasili nchini Kenya na kupitia ukurasa wake wa Twitter

Kiongozi wa Wakatoliki duniani, Papa Francis wa Kwanza amewasili leo Kenya kuanza ziara ya siku tatu ambapo Ijumaa atakwenda Uganda.

Baba mtakatifu Francis amewasili nchini Kenya na kupitia ukurasa wake wa Twitter, Papa Francis aliandika kwa lugha ya Kiswahili “Mungu abariki Kenya! God bless Kenya.”

Kuwasili kwake ni kuanza kwa ziara yake ya barani Afrika  Kenya, Uganda na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Baada ya kuwasili mjini Nairobi leo, papa atakutana na Rais Uhuru Kenyatta na kundi la Wanadiplomasia huko Ikulu.

Hapo kesho atakutana na kundi la watu wenye imani tofauti katika ubalozi wa Vatican katika mji mkuu wa Kenya.

Baadaye atafanya misa katika chuo kikuu cha Nairobi.

Siku ya Ijumaa papa atatembelea watu masikini mjini Nairobi katika eneo la Kangemi na kukutana na vijana katika uwanja wa Kasarani.

Leave A Reply