The House of Favourite Newspapers

Papa Francis kutua kwa kishindo Nairobi jioni leo

0

151125093646_pope_francis_boards_plane_512x288_afpPapa Franci akipanda ndege yake uwanja wa ndege wa Fiumicino, Roma kuelekea Nairobi Kenya.

Hii itakuwa ziara yake ya 11 akiwa kama papa nje ya Vatican.
Pia, katika ziara hiyo, Papa anaambatana na Waziri wa Mambo wa Nje wa Vatican, Kadinali Pietro Parolini na naibu wake, Angelo Becciu.
Ziara hii inatarajiwa kufuatiliwa na viongozi mbalimbali duniani kutokana na umashuhuri wa kiongozi huyo.
Papa Francis kabla ya kuja barani Afrika, hivi karibuni alifanya ziara katika nchi za Cuba na Marekani.
Serikali ya Kenya imetangaza kuwa kesho itakuwa siku ya mapumziko ambayo pia itatumiwa kama siku ya kitaifa ya maombi ya kujitafakari.
Nairobi, Kenya. Serikali ya Kenya inatarajia kukuza uchumi kwa takriban kiasi cha bilioni mbili katika kutokana na ziara ya Papa Francis inayofanyika leo nchini humo.

151125121108_pope_francis_airborne_to_kenya3_512x288_reuters_nocreditMtendaji Mkuu wa Biashara na Utalii, Anna Othoro alisema zaidi ya watu milioni 1.5 kutoka sehemu mbalimbali wanatarajia kuhudhuria ibada maalumu itakayoendeshwa na Papa Francis.

Alisema kuwa wageni wengi wamewasili kiasi cha kufanya hoteli nyingi kufurika jambo linaloashiria kuongezeka mapato kwa wafanyabiashara.

Pia, alisema ziara ya Papa Francis itabadilisha sura ya Nairobi kutokana na ugeni ambao ataambana nao.
Papa Francis leo anaanza ziara ya kihistoria Kenya pia Ijumaa atakwenda nchi jirani ya Uganda.
Ziara hiyo inafanyika baada ya kupita miezi michache tangu Rais Barack Obama wa Marekani kutembelea nchi hiyo.

Kwenye ziara hiyo ya siku sita itakayomfikisha pia katika nchi za Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati, Papa Francis anatarajiwa kutoa ujumbe wake wa amani, maridhiano, mashauriano na kuchochea juhudi za kuzima migawanyiko.

Mataifa yote matatu yamekuwa yakijiandaa kumkaribisha kiongozi huo wa Kanisa Katoliki duniani na msisimko mkubwa unashuhudiwa kote.
Hii itakuwa ziara ya 11 ya Papa Francis akiwa nje ya Vatican.

Leave A Reply