Papaa Msofe Kortini kwa Tuhuma za Kuongoza Wahalifu – Video

Wafanyabiashara wanne akiwemo Marijan Msofe maarufu kama Papaa Msofe na Wakili wa Kujitegemea Mwesigwa Mhingo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na Mashtaka Matano ikiwemo Kuratibu Genge la Uhalifu, Utakatishaji Fedha na Kujipatia Fedha kwa Njia ya udanganyifu.

 

Wakili mwandamizi wa Serikali Ladslaus Komanya amedai washtakiwa wanadaiwa kufanya makosa hayo kati ya Desemba 2018 na Septemba 2019 ndani ya Jiji la Dar es Salaam ambapo walijipatia zaidi ya Shilingi Milioni 900.

 

washtakiwa walijipatia Fedha hizo kwa madai ya kumuuzia Dhahabu kg 200 John Manson na kumsafirishia hadi nchini Ureno wakati wakijua si kweli na kati ya Septemba 2019 washtakiwa walimlaghai John Mahson kwa kumuuzia kg 20 za Dhahabu hali ikiwa ni uongo.

 

Baada ya kusikiliza Shauri hilo Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi amehairisha kesi hiyo hadi Desemba 16 mwaka huu kwa kuwa shauri hilo ni la uhujumu uchumi. katika kesi hiyo, washtakiwa wengine ni Wencelaus Mtui, Fadhili Mganga na Josephine Haule.


Loading...

Toa comment