The House of Favourite Newspapers

Parachichi ni tiba katika miili yetu

0

avocado-sliced-in-half.jpgWAKATI huu ni msimu wa tunda la parachichi Wazungu huliita avocado. Sehemu nyingi tunda hili linapatikana ama kwa kuuzwa tena kwa bei rahisi kwenye magenge au sokoni.

Parachichi lina kiwango kidogo cha majimaji ukilinganisha na matunda mengine. Linaweza kuliwa lenyewe au kwa kuchanganywa na matunda mengine kama tikitimaji, embe, ndizi au papai na kadhalika.

Wataalamu wa mambo ya afya wanasema parachichi linasaidia sana kwa afya ya akili. Tunda hili lina kiwango kidogo cha tindikali ambayo husaidia kukinga au kutibu maradhi.

Parachichi pia husaidia kukinga maradhi mbalimbali kama vile magonjwa ya moyo, kiharusi na maradhi ya kansa.

Wataalamu wanasema parachichi lina kiwango kikubwa cha Vitamini E kuliko ile inayopatikana katika mayai ambayo husifika kwa kuwa na vitamini nyingi.

Tunda hili pia lina Vitamini B6  ambayo husaidia sana kumpa nafuu mtu mwenye matatizo ya msongo wa mawazo kama ilivyo kwa Vitamin E lakini pia lina madini ya chuma na potassium.

Parachichi pia limethibitishwa kitaalamu kuwa ni tunda linalopunguza lehemu yaani cholesterol kutoka kwenye damu hasa kwa watu wanene.

Pia tunda hili husaidia kukuza na kuzifanya nywele zisikatike, kulainika na kung’arisha ngozi. Pia huweza kutumika na watu wengine kama siagi kwa kupaka kwenye mkate au wengine huchanganya kwenye wali au ubwawa au kusaga na kuwa juisi.

 Wanaopenda ngozi yao isikunjikekunjike hata wakiwa watu wazima wanashauriwa kula parachichi kila siku.

Maganda ya parachichi na mbegu yake watu wa tiba mbadala hutumia kutengeneza dawa ambayo inatibu wanawake ambao hawapati siku zao. Hata hivyo, hakuna uthibitisho wa dawa hizo kisayansi katika matumizi hayo.

Leave A Reply