The House of Favourite Newspapers

R.O.M.A: Kufanya kolabo siyo kiki!

0

15. Mwana Hip Pop kutoka Tanga Roma Mkatoriki ni moja kati ya watu waliofanya poa kwenye jukwaa hiloANDREW CARLOS

STAA wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘R.O.M.A Mkatoliki’ amefungukia madai ya wasanii wanaokimbilia kufanya kolabo nje ya nchi kwa kuamini kuwa itawapandisha kwenye chati haraka kuwa siyo kweli.

Akichonga na Showbiz Xtra, R.O.M.A anayebamba na Ngoma ya Kaa Tayari akishirikiana na Jose Mtambo na Darasa alisema kuwa, wasanii wengi hasa wa Bongo Fleva wamekuwa wakihaha kuhakikisha wanafanya kolabo za kimataifa kwa kuamini watapata kiki za fasta.

“Sijawahi kuona kiki za fasta kwenye gemu kama wanavyofanya wasanii wa Bongo. Wanachoshindwa kuelewa ni kufanya kitu kizuri kwanza nyumbani tena kukubalika kisha wao wenyewe kutoka nje watakuja kufanya kolabo na wewe,” alisema.

Leave A Reply