The House of Favourite Newspapers

Rais Barrow Kuwaachia Wafungwa wa Kisiasa, Kuibakiza Gambia ICC

adama

RAIS Mteule wa Gambia, Adama Barrow ameliambia Shirika la Habari la Associated Press (AP) kuwa atawaachia huru kutoka gerezani wanasiasa wote wa upinzani waliofungwa wakati wa utawala wa Yahya Jammeh anayeondoka madarakani.

Barrow amesisitiza kuwa atabadili pia msimamo wa awali wa Jammeh wa kutaka kuiondoa Gambia katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC, na Jumuiya ya Madola.

Aidha rais huyo aliyemshinda mpinzani wake huyo aliyekaa madarakani kwa miaka 22, amewahimiza watu walioikimbia Gambia kwa sababu ya hali ngumu ya maisha kurudi nyumbani ili kusaidia kulijenga taifa lao.

Baada ya kutangazwa kuwa mshindi, raia wengi wa Gambia walikesha usiku kucha wakisherehekea kuondoka kwa Bw Jammeh madarakani, ambaye amesema kuwa ataendelea na shughuli zake za kilimo.

Taifa la Gambia ni miongoni mwa nchi masikini, na wananchi wake wengi wamekimbilia mataifa ya ng’ambo.

halotel-strip-1-1

Comments are closed.