JPM: Jengo la Serikali Msingejenga kwa Bil. 10 – Video
RAIS John Magufuli leo Jumatatu, Novemba 25, 2019 ameweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Bodi ya Usajili wa Makandarasi Jijini Dodoma.
“Sina uhakika kama hili lingekuwa la serikali lingejengwa kwa Sh. bilioni 10, pangewekwa mambo mengi. Ninafahamu huwa kuna tatizo lingine ingawaje halikuwa sana, mnapo-tender kuna baadhi ya document huwa zinachomolewa na baadhi ya mainjinia ambao sio wazuri,” alisema Magufuli na kuendelea:
“Ninawajua makandarasi, ninajua shida zenu, ninajua mateso yenu, tumieni nafasi hii, ninawaambia kwa dhati. Makandarasi wazalendo mnaweza; hakuna nchi duniani ambayo haiwasaidii makandarasi wake, jipangeni ndugu zangu, mtafanya mengi makubwa kwa wakati huu.”
Comments are closed.