The House of Favourite Newspapers

Obama Ateketeza Bil. 25 Kununua Jumba la Kifahari

0

RAIS mstaafu wa Marekani, Barack Obama, na mkewe, Michelle Obama wamenunua jumba la kifahari lililopo eneo la Martha Vineyard katika Kisiwa cha Massachusetts kwa fedha za Tanzania Sh. bilioni 25 bilioni (Dola milioni 11.75).

 

Martha Vineyard ni eneo linalotumika kwa ajili ya mapumziko, na kiongozi huyo amewahi kwenda huko kwa ajili ya mapumziko wakati akiwa bado yupo madarakani. Kutokana na hilo, kabla hajalinunua jumba hilo, tayari kulikuwa na tetesi juu ya uwezekano wa yeye kufanya hivyo.

 

Familia ya Obama imenunua jengo hilo kutoka wa Wcliffe Grousbeck ambaye anamiliki klabu ya mpira wa kikapu ya Boston Celtic, na Corinne Basler Grousbeck.

 

Jumba hilo lenye nyumba saba vya kulala limekaa juu ya eneo lenye ukubwa wa takribani ekari 30 karibu na Ziwa la Edgartown Great. Bei ya awali ya jumba hilo ilikuwa Sh. bilioni 34.

 

 

 

 

Duh! TANASHA Alivyokata MAUNO, DIAMOND Akishuhudia, HARUSINI kwa DARLEEN…

Leave A Reply