The House of Favourite Newspapers

Rama Dee: ‘How come’ Jide awe mpenzi wangu?

0

IMG_5824Rama Dee

Mkongwe wa RnB Bongo, Rama Dee juzikati alipanda kwenye jukwaa na kuimba na Mwanamuziki Lady Jaydee pale Mlimani City, watu wasiomfahamu wakajua yeye ndiye mpenzi wa Jide kutokana na mabaha waliyooneshana.

Baada ya pale akawa amepokea sms na simu nyingi za mashabiki wake wakitaka kujua kama yeye ndiye mrithi wa Gardner maana Jide aliahidi kumuanika siku hiyo.

JIDEJide

Kufuatia usumbufu huo, Rama Dee ameamua kuifungukia safu hii na kueleza kuwa, Jide hawezi kuwa mpenzi wake ila ni msanii ambaye wamekuwa wakishirikiana kwenye mambo mengi na anampenda sana.

“Dah! Jamani how come mimi niwe mpenzi wa Jide? Wanaonijua wanafahamu kuwa ni kitu kisichowezekana ila yule ni mshikaji wangu wa long time, kimuziki na kimaisha pia,” alisema Rama Dee ambaye kwa sasa anaishi Autralia.

Leave A Reply