The House of Favourite Newspapers

RC Makonda Atoa Siku 14 kwa Ma-DC Kuwaondoa Machinga

rc-makonda-1 DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo ametoa siku 14 kwa Wakuu wa Wilaya za Jiji hili kuhakikisha machinga wote wanafanyia biashara katika maeneo waliyopangiwa.

rc-makonda-2“Kauli ya Rais aliyoitoa kwamba machinga wasibugudhiwi isitumike vibaya kwani hata wao hawapaswi kuwabugudhi wananchi wengine kwa kufanya biashara zao mbele ya maduka na barabarani,”amesema Makonda.

rc-makonda-3Ameongeza kuwa anatambua kuwa machinga wanajitafutia riziki lakini hawapaswi kuvunja sheria kwa kufanya biashara hata katika maeneo yasiyokuwa rasmi.

“Barabara zimejengwa kwa gharama kubwa hivyo haziwezi kubadilishiwa matumizi na kuwa sehemu ya machinga kupanga na kuuzia bidhaa zao” amesema.

Na Hilaly Daud/Gpl

Comments are closed.