The House of Favourite Newspapers

Rose Ndauka Azindua Lebo Ya ‘Ndauka Music’

rose-ndauka-1Ofisa Masoko wa Ndauka Adverts Ltd, Aneth Mosha (kulia) , akifuatiwa na msanii Casso na Mkurugenzi wa Ndauka Adverts Ltd, Rose Ndauka na meneja wa msanii huyo Ramadhani Mwanana.

rose-ndauka-2

Ramadhani Mwanana (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Rose Ndauka, Casso na Aneth Mosha wakiwa katika picha ya pamoja.

rose-ndauka-3Rose Ndauka na Casso wakipozi mbele ya kamera.

Na Mayasa Mariwata/GPL

STAA wa filamu Bongo,  Rose Ndauka, kupitia kampuni yake ya Ndauka Adverts Ltd, leo amezindua  lebo ya muziki iitwayo Ndauka Music ambayo itatoa fursa kwa wanamuziki nchini, hususan wanaochipukia,  ili kujitangaza.

Uzinduzi huo ulifanyika ofisini kwake Sinza, jijini Dar es Salaam, maeneo ya Sinza-Afrika Sana karibu na ofisi za Mamlaka ya Kodi (TRA) Mwenge, ambapo alimtangaza msanii wa Bongo Fleva, aitwaye Casso ambaye leo ameachia rasmi video ya ngoma yake iitwayo ‘Kitonga’.

Akizungumzz na waandishi wa habari,  Rose alisema ameichunguza sekta ya muziki  kwa kipindi kirefu pamoja na kumpika msanii huyo kwa muda usiopungua mwaka mmoja hadi kuamua kumtoa hivyo ana ujuzi na kile anachokifanya.

“Wengi wamenizoea kwenye filamu, lakini mbali na hilo mimi ni shabiki mkubwa wa muziki kwa hiyo naelewa kila kitu kuhusu hii fani, nimeamua nianze na huyu kwanza kisha wengine watafuata.  Wapo kama watatu kwenye lebo yangu lakini sitaki kuwatoa wote kwa mkupuo,” alisema.

Comments are closed.