The House of Favourite Newspapers

Rwanda na Burundi Zasitisha Usafirishaji Mafuta kwa Kutumia Bandari ya Mombasa, Kisa Uchakachuaji

bandariniNchi za Rwanda na Burundi zimetangaza kuacha kusafirisha mafuta kupitia bandari ya Mombasa nchini Kenya kwa madai ya vitendo vya uchakachuaji wa mafuta yao.

Sasa nchi hizo zitatumia Bandari ya Dar es salaam kusafirisha mafuta yao.

Kwa muda mrefu Bandari ya Mombasa imekuwa ikituhumiwa na wafanyabiashara wa mafuta kwa uchakachuaji.

Hatua inategemewa kugeuka mwiba mchungu kwa Bandari ya Mombasa kwa sababu ya kuondokewa na wateja wake muhimu wawili ambao walikuwa wakiingizia fedha za kigeni nchi yao.

Comments are closed.