The House of Favourite Newspapers

Sababu za ugumba kwa Mwanamke

0

evaluation-of-female-infertility1Mwanamke anachangia asilimia 40 katika tatizo la ugumba kwenywe ndoa. Sababu za ugumba kwa mwanamke zinaweza kuwa  ni historia kama amewahi kuwa kwenye uzazi wa mpango kwa muda mrefu Length of contraceptive.

Sababu nyingine ni idadi ya mimba na utoaji mimba Abortions, magonjwa ya zinaa kama nilivyokwisha yataja hapo awali na uvimbe katika tumbo la uzazi, mirija na mayai Myoma, Tubal or Ovarian masses.

Mwanamke anaweza kuwa na ugumba kutokana na kukosa tumbo la uzazi au kuwa na bikira Imperforated hymen au kutokwa na uchafu au maji kwenye uzazi Discharge.

Zipo pia sababu za ugumba kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume hizo ni kushindwa kugundua lini, muda yai la kike linapokuwa limekomaa Ovulation, kutambua kama Vulation imetokea.

Pia wahusika wajiuliza Je, mirija ya uzazi iko vizuri kuruhusu mbegu za kiume na yai la kike kukutana ili kutungishwa? Je, wanandoa wako vizuri kimwili na kisaikolojia kwa ajili ya kujiandaa kupata mimba?

TIBA NA USHAURI

Ni vizuri kumuona daktari ili aweze kuwasaidia kutambua lini yai la kike linakuwa limekomaa tayari kwa kutungishwa ili tarehe zinapokaribia basi mkutane kimwili.

Daktari atachukua vipimo vya damu kuangalia magonjwa ya zinaa, mkojo, vipimo vya shinikizo kubwa la damu, kisukari na joto la mwili.

Mwanamke atapimwa HSG Hysterosaloingography kuangalia mirija inayosafirisha mayai kama iko sahihi au imeziba kutokana na kadhalika.

Asilimia kati 15 hadi 20 ya wanandoa wenye tatizo la ugumba.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply