Safari Lager kuliteka soko na bia mpya ya kopo yenye ujazo wa 500ml
Kampuniya Bia ya TBL kupitia bia yake ya Safari lager imezindua bia yako poya kwanza yenye ujazo wa mili lita 500 kwa bia ya Kitanzania. Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar, Meneja Bidhaa wa Safari Lager, Edith Bebwa Nasuwa alisema “Ni bia ya kwanza ya Kitanzania ya kopo yenye ujazo wa mili lita 500 ambayo italeta urahisi, unafuu na ladha nzuri ya aina yake kwa wapenzi wote wa bia ya Safari Lager”
Bia hii ya kopo tayari imeshaanza kupatikana maeneo yote nchini kuanzia tarehe 26 Agosti 2016 na imeelezewa kuwa ni bia ya wajanja wenye kujiamini.
“Bia mpya ya kopo ya Safari nidhahiri kwamba imetengezwa kumpa umahiri Mtanzania katika safari ya maisha yake. Inapatikana kwa urahisi na kwawakati muafaka hat awakati mtu anakwenda kwenye mihangaiko yake au kubeba akiwaa na kwenda kwenye matembezi au safarini” alimalizia Edith Bebwa.
Fuatilia kurasaza Safari Lager kupata habarizaidi
Facebook: https://web.facebook.com/SafariLagerTz
Instagram: https://www.instagram.com/safarilager_tanzania/