The House of Favourite Newspapers

Salama: Nilimdis MwanaFA, Akanimaindi Kinoma!

0

salama4Salama Jabir.

UKIAMBIWA umtaje Muasisi wa Kipindi cha Planet Bongo cha EATV ambacho enzi ana-kifanya kilicha-ngia ubora wa video za Muziki wa Bongo Fleva nchini kukua kutokana na kasumba yake ya kuzikosoa bila woga, moja kwa moja utamtaja Salama Jabir ‘EceJay’.

Pia ukikutana naye, Salama ni mcheshi, mtundu na ana ufahamu mkubwa katika masuala ya burudani. Kama ulishawahi kufuatilia Vipindi vya Mkasi, Ngazi kwa Ngazi na Shindano la Bongo Star Search (BSS) namna ya uulizaji wake wa maswali kimtego utaku-baliana nami.

Mwi-shoni mwa wiki iliyo-pita, Salama alifa-nyiwa maho-jiano katika Kipindi cha The Playlist cha Omary Tambwe ‘Lil Ommy’ kinachorushwa kupitia Radio Times FM na katika makala haya yanaanika mahojiano hayo;

Ommy: Ngoma yako unayoikubali zaidi ni ipi?

Salama: Ahahaa! Jana (Ijumaa) ujue nilikuandikia meseji, sasa nilikuwa nimeshiba kichizi na nilikuwa nimekaa kwenye kikochi changu f’lan hivi cha tafakuru ambacho ukikaa lazima madini yashuke! Nikakwambia nipigie Malome ya Cassper Nyovest alioshirikiana na kikundi cha wamama wa kizamani sana wanaitwa Mahotela Queens.

Ommy: Kwa nini unaikubali ngoma hii?

Salama: Ina ubunifu uliopitiliza, ujue wasanii wengi wa Hip Hop wanapenda kufanya kazi na wanamuziki wa R&B au wanamuziki wenzao wa Hip Hop. Wiki mbili tatu zilizopita nilienda Sauz na AY nikakutana na hawa wamama, huwezi amini Ommy, hawajui kabisa Kiingereza maana niliwafuata na kuwaambia nawapenda nimekuwa nikiwaona tangu wanakua, sasa baadaye meneja wao (Mzungu) alinifuata na kuniambia; ‘ulikuwa unaongea nini maana wanakudiskasi’ ndiyo nikajua kumbe hawakunielewa.

Ommy: Umegusia Sauz, kule ulienda kufanya nini?

Salama: Nilikuwa na AY ambaye alienda kupafomu kwenye shoo moja ya uwanjani ya bure, wenzetu huwa wanafanya sana kwa makampuni makubwa kurudisha kwa jamii. Kulikuwa na wasanii wakubwa kutoka Afrika na pia ilikuwa inakaribia bethidei ya Mandela.

Ommy: Hamkuingiza vitu maana sehemu kama hizo za fursa?

Salama: Yeah jambo lilikuwepo, nilikuwa na AY na Hermy B hivyo siyo vizuri nilizungumzie sana maana wenyewe wapo watalizungumzia.

Dah nimekumbuka Ommy, hongera bwana kwa kufunga ndoa, umechukua kitu nanii kabisa, hutaki kabisa kujifichaficha!

Ommy: Ahahaa! Ujue Insta na Facebook zilikuwa nyingi sana mara Tambwe vipi, baby sijui nini!

Turejee kwenye swali, tumeona upo karibu sana wa AY na ikumbukwe kuwa AY ni mshkaji sana wa FA, lakini zamani mshkaji wako wa karibu sana alikuwa FA na ukaribu wako na FA ukasababisha kujuana na AY.

Salama: Dah! Yaani umenipeleka mbali kishenzi, kwangu huwa sina za kubondibondi, kama ni mshkaji wangu ni mshkaji na kama siyo siyo tu. Ujue mimi kuwa rafiki na mtu ni ngumu sana na urafiki huwa unatoka kwenye roho, tangu nimekua, marafiki zangu miaka nenda rudi ni haohao (AY na FA) na pia ni marafiki kibiashara.

Ommy: Ulikuwa mkosoaji sana video za Kibongo, unafurahia video za sasa?

Salama: Nafurahi kuona tumetoka sehemu moja kwenda nyingine na tupo mbali ukilinganisha kwa nchi nyingine kwa maana ukiangalia wanavyoimba na ukiangalia video zao duh, sijui wapo dunia ya wapi.

Ommy: Vitu gani haviko sawa katika video za Kibongo?

Salama: Kama nilivyosema, kwanza inabidi tujikubali kwa hatua tuliyofikia. Ubunifu ni suala lingine, tusikariri sana utakuta video jamaa amekutana na demu akanunua nyanya.

Ommy: Unakumbuka nini katika kukosoa kwako?

Salama: Nakumbuka ilikuwa Video ya Nakomaa Nao, mimi nikachambua kuwa FA hakupiga pasi suti yake, dah kuna siku nilikuwa nimesha-sahau nikakutana nao pande za Morocco nikasa-limiana nao lakini FA akani-chunia. Baada ya siku kadhaa nikakutana na AY akaniambia jamaa alinichunia kwa kuwa nilimsema kwenye video hajapiga pasi.

Leave A Reply