The House of Favourite Newspapers

Samatta aanza kazi rasmi

0

samataMbwana Samatta.

Omary Mdose,Dar es Salaam

KWA mara ya kwanza straika, Mbwana Samatta, juzi Jumamosi aliandika historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu Ulaya, baada ya kuiongoza timu yake ya Genk kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mouscron-Péruwelz katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Samatta aliingia dakika ya 73 kuchukua nafasi ya Nikos Karelis raia wa Ugiriki, ambaye pia amesajiliwa kwenye dirisha hili dogo akitokea Panathinaikos ya nchini kwao.Bao pekee la kina Samatta lilifungwa na Thomas Buffel dakika 64 na kuipaisha hadi nafasi ya tano kwenye msimamo, ikifikisha pointi 38 katika michezo 25 katika ligi yenye timu 16 kama Ligi ya Tanzania Bara.

Genk imeshinda mechi 11, sare tano na kuchezea vichapo tisa katika ligi inayoongozwa na Gent yenye pointi 52, tatu mbele ya Club Brugge inayoshika nafasi ya pili.

“Napenda kuchuna fursa hii kuwashukuru Watanzania pamoja na mashabiki wangu wote wa Genk kwa maombi na sapoti yenu, leo (juzi)nimefanikiwa kucheza mchezo wa kwanza rasmi na klabu yangu ya Genk na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0,” aliiandika Samatta kwenye akauniti yake ya Instagram.

Leave A Reply