Sapraizi ya Askofu Gwajima Yaacha Gumzo – Video

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini Tanzania, Dr.Josephat Gwajima Ameahidi Kumpatia Shilingi Milioni 100 Muimbaji Wa Muziki Wa Muziki Wa Injili John Lisu Lengo ikiwa ni Kumsapoti katika Huduma Yake Ya Uimbaji na Kufanya Vizuri zaidi.

Askofu Gwajima ameyasema hayo Jana Katika Kanisa la CCC Upanga Dar es Salaam ambapo Muimbaji John Lisu alikuwa akifanya Live DVD Recording Inayoitwa “MTAKATIFU”

Askofu Gwajima ameongeza kuwa atatafuta group la marafiki zake na ambao nao watatoa Milioni 100 ili kufikisha Milioni 200 ambazo atampatia John Lisu ili kufanikisha mahitaji katika huduma yake ya uimbaji hapo mwakani 2020 na kwa mchango wake huo amemtaka John Lisu ashindwe mwenyewe kufanya mambo makubwa mwakani.


Loading...

Toa comment