The House of Favourite Newspapers

Shigongo, Prof Mkumbo Kivutio Mafunzo Ya Wahitimu Kidato Cha Sita Dar

0

1

Wahitimu wakiendelea kupata mafunzo kutoka kwa wahamasishaji.

2

Wahitimu wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakiendelea.

3

7

4

Mafunzo yakiendelea.

5

Mfundishaji, Dkt. Haruni Nyagori akiwafundisha wahitimu kidato cha sita mbinu mbalimbali za elimu ya juu.

6

Dkt. Nyagori akiwafafanulia mambo mbalimbali yanayohusu elimu ya chuo kikuu.

8

Prof.Kitila Mkumbo akifanya mahojiano na wanahabari baada ya kuhitimishwa mafunzo hayo.

9

Eric Shingongo akisalimiana na Prof. Mkumbo baada ya kuwasili ukumbini hapo.

10

Prof. Mkumbo akiwapa mbinu mbalimbali za mambo muhimu ya Elimu ya Chuo Kikuu wahitimu Kidato cha sita.

11

Mmoja wa wahitimu kidato cha sita akiuliza jambo kutaka ufafanuzi kutoka kwa watoa mada.

12

Eric Shigongo akiimba Wimbo wa Tanzania Nakupenda pamoja na wahitimu kidato cha sita waliofika kwenye mafunzo ya kupata mbinu za kujiunga na Elimu ya Chuo.

13

Washiriki wakimsikiliza Shigongo.

14 15

Eric Shingo akiwapa mbinu mbalimbali za mafanikio yao kuelekea wanapoenda chuo ili waweze kuondokana na dhana potofu.

16

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo akihojiwa na wanahabari baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.

MAFUNZO ya wahitimu kidato cha sita kutoka shule mbalimbali hapa nchini yaliyoanza Jumamosi, yalihitimishwa juzi Jumapili na kuwa kivutio kwa wanafunzi waliojitokeza kwa wingi kupata mbinu za namna ya kuelekea kuchagua kozi zao za Elimu ya Chuo Kikuu.

Mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika katika Ukumbi wa Nkurumah uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) yalikuwa yakiwaandaa wanafunzi hao kabla ya kuelekea elimu ya chuo kikuu.
Miongoni mwa wazungumzaji waliohitimisha  mafunzo hayo walikuwa ni, Prof, Mkumbo, Ofisa Mwandamizi wa Habari Elimu na Mawasiliano kutoka katika Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu, Veneranda Malima, Dkt. Harun Nyagori kutoka Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Omega Ngole kutoka Bodi ya Mikopo na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo ambaye ndiye alihitimisha mafunzo hayo.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Shigongo alisema kuwa anaimani mafunzo hayo yatakuwa na tija kwa wanafunzi hao kwani maarifa waliyopata kutoka kwa wahamasishaji wote wakiyatumia vyema basi watanufaika kwa maisha ya baadaye.

“Ninyi wahitimu hakikisheni mnafanya mambo kwa usahihi ili kujikwamua kutoka kwenye maisha magumu na kuja kuinua kipato cha nchi,” alisema Shigongo.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply