The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba… Utaamini mwenzio atakapopewa nyumba!

0

Nyumba (9)Washindi wa droo ndogo ya shinda nyumba

Na Mwandishi Wetu

UMEAMKA zako kama ulivyolala jana, mawazo yako yote yapo juu ya nini utafanya ili kukabiliana na mwaka huu mgumu, ambao waswahili wanasema eti Rais John Pombe Magufuli, amebana kila upenyo wa hela, yaani ni mwaka mgumu.

Ghafla simu yako inaita na unapotazama kioo, namba huifahamu. Kwanza unasita kupokea kwa sababu unadhani ni Mama Ntilie uliyemkopa tangu juzi na umekata mguu kwake. Unaamini ametumia namba ya mtu mwingine kwa sababu simu zake tatu hujapokea.

Halafu unawakumbuka na wadeni wako wengine, maana kwa wiki nzima hujapokea simu za watu wote wanaokudai, ambao uliahidi utawalipa wiki hii. Ukiwa bado unawaza, simu inakatika, unaisoma namba na kuiandika pembeni. Dakika tatu mbele, namba ileile inapiga tena kwenye simu yako, unapiga ishara ya msalaba na kubonyeza kitufe cha kupokelea simu, potelea mbali liwalo na liwe, Mwenyezi Mungu nisaidie!

Sauti usiyoifahamu inakusalimia kwa taadhima, kisha inakuuliza kama wewe ndiye mwenye simu hiyo, unapokubali, inakuuliza kama katika siku za hivi karibuni umewahi kucheza bahati nasibu ya aina yoyote.

Unafikiria haraka na kukumbuka kuwa ulishanunua kuponi nyingi za Shinda Nyumba na Global Publishers, unajibu ndiyo, halafu mtu huyo anakuuliza jina lako hasa ni nani. Ukijua huenda ni zile zawadi ndogondogo za Tv Flat Screen au pikipiki (maana huamini kama kweli mtu atashinda nyumba, unajua hizo zawadi wanapeanaga wenyewe), unalitaja kikamilifu kama ulivyoandika katika kuponi zako.

Kwa mshangao wako, unaulizwa katika ushiriki wako ulitarajia kushinda nini, unajikanyaga kwa sababu hujui lengo la muuliza swali, unahofu huenda unaweza kuwa umeshinda kitu kikubwa lakini ukataja kidogo na wewe utapewa hicho hicho, hivyo unajibu kwa kujiamini “Nilitaraji kushinda nyumba.”

Ndipo unapoambiwa umshukuru Mungu, kwani sala zako zimesikilizwa na wewe ndiye mshindi wa droo kubwa kabisa kuwahi kutokea, ya Shinda Nyumba na Global Publishers na sasa wewe ndiye mmiliki wake halali!

Sina uhakika nini kitakutokea, lakini iwapo hali hiyo ingenikuta mimi, ambaye kwa bahati mbaya siruhusiwi kushiriki shindano hili kwa vile nina uhusiano na kampuni (Kumbuka, wafanyakazi wote wa Global Publishers na familia zao hawaruhusiwi kushiriki shindano hili) ningezimia, yaani network ingekata kwa muda!

Kama hauamini, shauri yako maana unajipoteza mwenyewe. Utakuja kuamini utakaposikia mtu unayemfahamu, amejishindia nyumba hii yenye thamani ya shilingi milioni 60.

Nyumba hii ni ile ya Global Publishers iliyopo Salasala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, inayotokana na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, itakayochezeshwa Juni 30, mwaka huu. Utashinda kwa kununua kuponi zilizopo kwenye magazeti yanayochapishwa na kampuni hiyo, ambayo ni Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi, Risasi na Amani.

Kwa shilingi mia tano tu, mtu unaweza kujikuta ukiondoka katika adha ya kuishi nyumba za kupanga na kuwa miongoni mwa watu wanaoitwa wenye nyumba.

Wapo baadhi ya watu wanakatisha wenzao tamaa kwa kuwaambia kuwa Global Publishers haiwezi kutoa nyumba. Niwathibitishie kwamba tukio hili ni la kweli na litatokea Juni 30, mwaka huu wakati wa uchezeshaji wa droo kubwa.

Kampuni hii pia imewahi kutoa zawadi kubwa za magari kama Mercedes Benz, Toyota Prado, Toyota Noah, Toyota Vitz na Fun Cargo, achilia mbali zawadi kama pikipiki za kila aina, vyombo vya nyumbani, seti za televisheni za kisasa na vitu vingine kedekede.

Leave A Reply