The House of Favourite Newspapers

Shirika la Ndege Etihad Lateua Mkurugenzi Mpya Nigeria

0

????????????????????????????????????

Mkurugenzi Mtendaji mteule wa Shirika la Ndege la Etihad nchini Nigeria Bw. George Mawadri.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Shirika la Ndege la Etihad ambalo ni shirika la ndege la taifa katika falme za kiarabu limemteua George Mawadri kuwa Mkurugenzi mpya wa shirika hilo nchini Nigeria, ambapo atahusika na kusimamia shughuli za usafiri wa ndege za Etihad na biashara ya usafari wa anga na kuimarisha biashara hiyo nchini Nigeria

Mkurugenzi huyo mpya amekuwa na uzoefu katika sekta hiyo ya usafirishaji. Amefanya kazi katika Shirika laNdege la British Airways kwa miaka 19 akiwa nchini Uganda, Kenya na Zambia pamoja na kutoa huduma katika nchi za Zimbabwe, Malawi, Ethiopia, Rwanda, Sudan na Sudan Kusini.

Nimefurahia uteuzi kwenye nafasi hiyo muhimu katika Shirika Ndege la Etihad katika sehemu ya sekta ya anga inayokuwa kwa kasi” Alisema Mawadri. Nitafanya kazi kwa ushirikiano na kuwa mbunifu ili kuongeza ufanisi katika shirika letu, kupanua masoko na kuwapa wateja wetu huduma bora.

Makamu wa Rais wa Shirika la Ndege la Etihad, Danny Barranger alisema “Nina furaha na imani kwamba George ataongoza vyema timu yetu iliyopo Nigeria ili kuongeza soko la biashara yetu nchini humo. Uzoefu wake kwenye biashara hii na rekodi yake ya mafanikio katika sekta ya anga Afrika na maeneo aliyofanya kazi ni jambo ambalo litamwezesha kuendeleza kuongeza ufanisi katika shirika la Etihad ambalo liliona umuhimu wa kumuweka katika nafasi hiyo.

Shirika la Ndege la Etihad lilizindua safari zake kati ya Lagos na Abu Dhabi 1 Julai 2012 na hivi sasa kuna safari nne kwa wiki kwa kutumia ndege ya Airbus A330-200 yenye uwezo wa kubeba abiria 254 ambapo daraja la kati abiria 18 na daraja la uchumi abiria 236.

—————
Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika hili lilianza shughuli zake mwaka 2013 hadi mwaka 2015 lilikuwa limetoa huduma ya usafiri kwa abiria jumla milioni 17. Shirika la Etihad lenye makao makuu yake Abu Dhabi hutoa huduma ya usafiri kwa abiria na vifurushi/mizigo katika nchi za mashariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia, Amerika n.k. Shirika lina aina mbalimbali za ndege Airbus 122, zikiwamo Boeing 204 zilizo kwenye oda ambazo ni pamoja na:- 71 Boeng 787s, Pia 25 Boeng 77Xs, 62 Airbus A350s na 10 Airbus A380s.

Shirika la Ndege la Etihad pia limewekeza katika Air Berlin, Air Serbia, Air Seychlles, Alitaria, Jet Airways, Virgin Austalia, na Uswisi- Darwin Airline.

Shirika la Etihad kwa kushirikiana na Air Berlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihadi Riginal, Jet Airways na NIKI pia wanashirikina na Etihad sekta ya usafiri wa anga jambo linalowawezwesha wateja wao kuwa na uwezo wa kuchagua huduma waitakayo kupitia ushirikiano huo na kuwawezesha kuboresha biashara hiyo kwa wateja.

Kwa maelezo zaidi tafadhari tembelea ukurasa wa www. etihad.com

Leave A Reply