The House of Favourite Newspapers

Shirika la Ndege la Etihad Kutumia  ‘Boeing 787’ Safari  za Tokyo

airbus_a330-202_etihad_airways_jp5752534

  • Boeing 787 Dreamliner inatoa huduma bora za daraja la kwanza na kawaida
  • Boeing 787 ndiyo ndege ya kifahari katika Shirika la Ndege la Etihad
  • Kuanza safari yake ya kwanza kutoka Abu Dhabi kwenda Tokyo Narita
  • Inahudumiwa na wahudumu mahiri katika fani za upishi, vinywaji na malezi

Kuanzia Desemba, mwaka huu Boeing 787 itaanza rasmi safari zake kati ya Abu Dhabi na Tokyo Narita  ikiwa imeboreshwa zaidi.

Ndege hiyo yenye daraja la kwanza, kati na daraja la kawaida inachukua nafasi iliyoachwa na ndege ya Airbus A340, ambayo kwa sasa imepangiwa vituo vingine tofauti kwa safari  za kila siku.

Ofisa mkuu wa Mipango na Mikakati wa Shirika la Etihad Kevin Knight amesema, “Ktumia ndege hiyo katika safari za Tokyo, ni kielelezo cha kutambua umuhimu wa kituo hicho cha Japan, pia ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati iliyowekwa na Shirika la Etihad.”

 Aliongeza kuwa “Ubora wa huduma zinazotolewa katika ndege hiyo, unaongeza thamani yetu katika ushindani wa masoko ya huduma za anga.”

Ndege ya Boeing 787 ina jumla ya viti 235. Kati ya viti hivyo, 8 vipo katika daraja la kwanza, 28 daraja la kati na 199 vya daraja la kawaida.

Viti katika daraja la kwanza vimeboreshwa kwa kuongezewa nafasi ya kutosha huku zikinakshiwa na kitambaa laini cha Poltrona Frau. Viti hivyo pia huweza kutumika kama vitanda ambavyo huweza kubeba mpaka watu wawili. Huduma zingine katika daraja hilo ni runinga na chakula kinachotolewa kwa oda maalumu.

Katika daraja la kati, wateja hupewa fursa ya kuchagua aina tatu za vyakula. Wahudumu wa vyakula na vinywaji pia wanatoa ushauri kwa abiria kuhusu aina ya chakula pamoja na vinywaji maalumu.

Abiria katika daraja hili pia wamewekewa mavazi maalumu pamoja na viatu vya wazi na sanduku maalumu lenye vifaa vya kutumia mtu binafsi..

Ndege hiyo pia imesheheni vifaa mbalimbali vya burudani kama vile Panasonic eX3 ambayo ina chaneli saba za televisheni, video, michezo na huduma ya mtandao unaotumia Wi-Fi pamoja na mfumo wa USB kwa kila kiti.

Huduma hii mpya inajumuisha wafnyakazi kutoka mataifa mbalimbali wakiwamo watumiaji wa lugha ya Kijapani. Wasaidizi wa kulea watoto pia wanapatikana katika kila safari ya  Boeing 787 ili kutoa msaada wa malezi.

Shirika la Etihad lilianzisha safari za kwenda Japan Februari,2010 ikiwa na ndege ya kila wiki kwa safari za AbuDhabi na Nagoya kupitia Beijing. Ratiba hiyo ilibadilishwa na kuwa ya kila siku Machi 2014 wakati safari za Tokyo Narita zikiongezwa katika ratiba ya Japan mwaka 2010 kwa kutumia ndege za kila wiki na kwa safari za kila siku mwaka 2013.

Ratiba ya ndege kati ya Abu Dhabi na Tokyo Narita, itakayoanza rasmi Desemba 2016

 

 

Namba ya ndege

Mwanzo

Muda wa

Kutoka

Kituo

Muda wa

Kufika

Mzunguko

Aina ya ndege

EY878

Abu Dhabi

04:10

usiku

Tokyo Narita

07:05

mchana

Kila siku

B787-9

EY871

Tokyo Narita

03:25 usiku

Abu Dhabi

10:45

jioni

Kila siku

B787-9


Muhimu
: Safari zimeorodheshwa kwa kuzingatia muda wa eneo husika.

Comments are closed.