The House of Favourite Newspapers

Simanzi na Vilio! Mazishi ya Bi Cheka – Video

0

HATIMAYE mwili wa mwanamuziki wa bongo Fleva, Cheka Haji maarufu kama Bi Cheka umehifadhiwa kwenye Makaburi ya Kigofu Bunju, jijini Dar es Salaam.

 

Kabla ya mazishi mwili wa Bi Cheka uliswaliwa nyumbani kwake Bunju B saa 7 mchana na saa 10 jioni kupelekwa makaburini.

 


Waombolezaji walianza kumiminika toka asubuhi na hadi jioni muda wa kuzika idadi yao haikuwa kubwa.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Bunju B, Hassani Selemani Mnondwa ndie aliyekuwa anaongoza Kamati ya Mazishi na swala aliswalisha Shekhe Mwinyi Gogo.

 

Kwenye mazishi hayo wasanii waliohudhuria ni Aslay na Meneja wake Chambuso, Beka Flavor na Mh Temba .

 

Tukio ambalo liliwashangaza watu waliohudhuria makaburini ni kukatazwa kwa Aslay baada ya kutaka kushika Koleo na kuweka mchanga kwenye kaburi la Bi Cheka.

Hadi mwisho wa mazishi hakuna hata msanii mmoja aliyeitwa kuweka mchanga katika kaburi zaidi ya ndugu na jamaa wa Bi Cheka. Bi Cheka alizaliwa mwaka 1959, Ilala jijini Dar es Salaam, ameacha watoto wawili Kombo na Adam na wajukuu 12.

 

Leave A Reply