The House of Favourite Newspapers

Simba ikiingia mtego huu imekwisha

0

KOCHA Hans van Der Pluijm amesisitizia wachezaji wake kucheza mipira ya chini kila wanaposhambulia na mwisho wa kucheza mipira ya juu ni katikati ya uwanja tu.

Kuanzia katikati kwenda mbele washambuliaji wa Yanga wameelekezwa kutuliza na kuizima mipira yote ya juu na kuweka chini kisha kucheza soka la kuonana hadi golini.

Katika mazoezi ya Yanga siku zote kisiwani hapa, Pluijm ameonekana akiwasisitizia  wachezaji wake kucheza mpira chinichini muda wote na hata krosi zao nyingi zilikuwa za chini.

Washambuliaji wa Yanga walionekana kuuzoea mfumo huo jambo lililoonekana kumfurahisha Pluijm na msaidizi wake, Charles Mkwasa.

Katika mazoezi ya juzi, viungo na washambuliaji wa Yanga walionekana kucheza kwa ufasaha mtindo huo anaoutaka kocha wao kiasi cha kupongezwa kila walipokuwa wakipata bao.

Kwa vyovyote vile, Yanga itautumia mfumo katika mchezo wake wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Leave A Reply