The House of Favourite Newspapers

Aliyekuwa Kocha wa Nigeria Stephen Keshi Kuzikwa Julai 29

0

KeshiMAZISHI ya aliyekuwa Kocha Mkuu na nahodha wa Timu ya Taifa ya Nigeria (Super Eagles) Stephen Keshi, aliyefariki Juni 8 mwaka huu, yatafanyika  Julai 29 nyumbani kwao mjini Illah, Oshimili Kaskazini, Jimbo la Delta.

Nigeria's national football team head coach Stephen Keshi watches on June 3, 2012 his team play a 2014 World Cup qualifying Group F match against Namibia at the U.J. Esuene stadium in Calabar. AFP PHOTO / PIUS UTOMI EKPEI (Photo credit should read PIUS UTOMI EKPEI/AFP/GettyImages)Kwa mujibu wa Kamishna wa Habari wa Delta, Patrick Ukah, ambaye ni mjumbe wa kamati ya mazishi ya Keshi, shughuli za mazishi hayo zitaanza Julai 28 na kumalizika Julay 31.

Pamoja na kuwepo na sala maalum katika Kanisa Katoliki na shughuli mbalimbali za maombi, patakuwepo pia na mechi ya soka itakayohusisha nyota mbalimbali nchini humo. ikiwa ni pamoja na kutolewa kwa heshima maalum kwa marehemu ambaye aliwika katika soka.

Leave A Reply