The House of Favourite Newspapers

Trump Kusitisha Uagizwaji wa Ndege Mpya za Air Force One

a-deal-for-donald-trump-b

Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump amesema anataka kufuta ombi la ununuzi wa ndege mpya za Air Force One ambazo hutumiwa na marais wa Marekani.

Wiki sita kabla ya kuchaguliwa, aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa: “Boeing wanaunda ndege mpya aina ya 747 Air Force One za kutumiwa na marais siku zijazo, lakini gharama yake imezidi, zaidi ya $4 billion. Futa oda hiyo!”

boeing

Serikali ya Marekani iliingia kwenye mkataba na kampuni ya Boeing ili kutengenezwa kwa ndege hizo mbili au zaidi za kuwabeba marais.

Ndege hizo zilitarajiwa kukamilika na kuanza kutumiwa mwaka 2024.

Hisa za kampuni ya ndege ya Boeing zilishuka kwa zaidi ya 1% baada ya ujumbe huo wa Trumpp kwenye Twitter, ingawa zilijikwamua baadaye.

Trump hatarajiwi kutumia ndege hizo mpya, iwapo hatashinda uchaguzi wa muhula wa pili wa mwaka 2020.

halotel-strip-1-1

MZEE WA MIAKA 76 ALEYETANAGAZA KUTAFUTA MKE “FULL EXLUSIVE INTERVIEW”

Comments are closed.