The House of Favourite Newspapers

Tutawanyoosha Kenya Chalenji Kesho Jumapili

0

WACHEZAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars wameapa kuwa iwe isiwe lazima wapambane ili waweze kupata ushindi wa kwanza kwenye michuano ya Chalenji dhidi ya Kenya, kesho.

Kilimanjaro Stars ipo Kundi B ikiwa na timu za Zanzibar, Sudan na Kenya na leo michuano hiyo inatarajiwa kuanza huko Kampala, Uganda na Kilimanjaro wao watacheza kesho Jumapili.

 

Wakizungumza na Championi Jumamosi, wachezaji wa Kilimanjaro, Juma Abdul na Bakari Mwamnyeto walisema kuwa, wamejipanga vema kupeperusha bendera ya taifa wana imani ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

“Tupo tayari kwa ajili ya kupambana na kupata matokeo chanya tunatambua kwamba ushindani ni mkubwa hilo halitupi shida kwa kuwa tumejiandaa kushinda mashabiki watupe sapoti pamoja na dua,” alisema Mwamnyeto.

 

 

Kwa upande wake Abdul alisema: “Tumejipanga vema na tumefanya maandalizi kiujumla, kila mchezaji anahitaji kuona timu inashinda, mchezo wa mpira ni ushindani tunawaheshimu wapinzani wetu tunajua kwamba nao wamejipanga kama sisi hivyo hatutawadharau.”

Leave A Reply