The House of Favourite Newspapers

Umuhimu wa mafuta ya nazi mwilini

0

MAFUTA NA NAZI

WENGI tunatumia nazi kama kiungo cha mboga kutokana na tui lake au wengine kutumia mafuta yake bila kujua faida yake kiundani.

Ndani ya tui la nazi kuna mafuta ambayo yana asidi muhimu iitwayo Lauric Acid ambayo ina uwezo mkubwa wa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti lehemu Kolesteroli mbaya kwenye moyo na mwili kwa ujumla.

 Lauric Acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalam kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalam kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni muhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalam wa lishe wa Lifesum.

Mafuta ya nazi pia huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula lakini pia yanao uwezo wa kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta ya wanyama, jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini.

Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo wa mwili kukimeng’enya chakula, watu wanaoyatumia mafuta haya kupikia vyakula vyao kila siku kwa kawaida huwa na uzito wa kawaida. Faida nyingine ya mafuta ya nazi ni kung’arisha ngozi. Kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye mwili wako.

Mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa wa kuua bakteria, virusi na vijidudu vya aina yoyote vinavyoweza kuidhuru ngozi. Unaweza kupaka mafuta haya mwili mzima hadi kwenye nywele na kwenye kucha au kuyatumia kwa ‘masaji’.

Mafuta ya nazi ni chanzo kizuri cha nguvu ya mwili kwani yana sifa yakuingia kwa kiasi kidogo kwenye damu Medium Chain Triglycerides – MCT’, sifa hii huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu au hubadilishwa kuwa Ketones ambacho ni chakula cha ubongo.  Mafuta haya hutibu pia tatizo la kupoteza kumbukumbu. Tafiti nyingi zimeonesha kuwa mafuta ya nazi yanao uwezo wa kuziamusha seli na shughuli za ubongo na katika kufanya hivyo husaidia kuzuia matatizo ya ukichaa Dementia na kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

 Mafuta ya nazi yana uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji kwa kupaka ndani ya pua.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply