The House of Favourite Newspapers

UN Yalaani Korea Kaskazini Kurusha Kombora la Masafa Marefu

0

korea (2)
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani hatua ya Korea Kaskazini kulipua Kombora la masafa marefu.

Katika taarifa iliyotolewa baada kikao cha dharura mjini New York imesema baraza limekubaliana kuiwekea nchini hiyo vikwazo vya kiuchumi mapema iwezekanavyo,lakini pia baraza hilo limeilaumu Korea Kaskazini kwa kukiuka maazimio ikiwa ni pamoja na hatua yake ya kulipua bomu la nyuklia mwezi January.

korea (3)Kauli hizo za kuilaani hatua hiyo Korea Kaskazini zimetowa maeneo mbali mbali duniani pamoja na kulaumiwa na dunia Korea Kaskani yenyewe imesema imelipua kombora hilo ili kutuma mitambo ya satellite angani,jambo linalopingwa na mahasimu wake kuwa hiyo ni danganya toto kwani ina nia ya kujaribu kombora angani.

korea (4)Akitoa taarifa ya kulaani hatua hiyo Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa ambaye pia ni Balozi wa Venezuela Rafael Ramirez Carreno amesema wanachama wamekubaliana kulaani kile alichosema ukiukwaji Korea Kaskazini wa azimio la Umoja wa Mataifa.

korea (5)Rafael Ramirez Carreno,amesema ”Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli wamelaani vikali hatua hii ya kulipua kombora hilo, wanachama wa Baraza la usalama la umoja wa mataifa wamesisitiza kuwa jaribio hilo na mengine ya ulipuaji yaliyofanywa na Korea Kaskazini ambayo yanatumia teknologia ya angani hata kama yana tabia kama ya ulipuaji mitambo inayofanana na ya satellite, yanachangia mfumo wa Korea Kaskani wa kulipua silaha za nyuklia ambayo ni hatari na inayokiuka azimio la Umoja wa Mataifa.

korea (1)Kwa upande wake balozi wa Marekani ndani ya Umoja wa Mataifa Samantha Power amesema hakuna mtu anayeweza kufanywa mjinga na Korea Kaskazini kwamba inalipua kombora kwa ajili ya mipango ya satellite na shughuli za anga.

Samantha Power, amesema kwamba “Ambacho Korea Kaskani imefanya kwa tukio hili, tukio ambalo ni kinyume cha sheria, katika matukio yote ya ulipuaji , ni ulipuaji wenye kuendeleza mipango ya Korea Kaskanini kuongeza uwezo wake wa kuendeleza utengenezaji wa silaha za nyuklia.

Hatua hiyo ya Korea Kaskazini imeelezwa kuwa sio tu ukaidi kwa moja ya matukio hayo, nchi hiyo inasonga mbele hatua moja katika kudhihirisha azma yake ya kuendeleza nyuklia yenye uwezo wa kuingia bara nyingine kwa kombora la angani, hili hatutalikubali wala hatutaruhusu hili kutokea.

Chanzo: BBC

Leave A Reply