The House of Favourite Newspapers

Unampenda? Muoneshe ‘valentine’ wako!

0

healthycouple-lifemagHeshima na utukufu ni kwake Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kukutana tena Jumatatu hii murua. Leo katika safu yetu ya XXLove tunazungumzia umuhimu wa mapenzi ya dhati kwa umpendaye katika kipindi hiki cha Valentine’s Day ambacho huadhimishwa kila Februari 14 na vipindi vingine vyote.

Kama kweli unampenda mpenzi wako, muoneshe namna unavyompenda, muoneshe vile alivyo wa thamani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kilele cha siku hiyo ya wapendanao.

Yawezekana hamkuwa vizuri na umpendaye kwa mambo f’lani, yawezekana mlikuwa na migogoro ya hapa na pale, basi jaribu kuifuta au kuimaliza katika msimu huu wa valentine ili muendelee vyema katika uhusiano wenu.

Yawezekana kabisa kuwa, wewe ndiye uliyeanza kumkosea au kumkwaza mwenza wako au ‘valentine wako’. Chukua hatua ya kumuomba msamaha. Ni jambo dogo sana ila lina maana kwa mwenza wako. Pata nafasi ya kukaa naye na kuzungumza naye kama una nafasi ya kumtoa ‘out’, fanya hivyo, mpeleke sehemu ambayo hajaizoea.

MSAMAHA
Mwambie: “Mpenzi, mchumba, mke au mume wangu, najua nilikukosea sana ila sina budi kukuomba msamaha, kwani bado nakupenda, nakuhitaji sana katika maisha yangu yaliyobaki hapa duniani. Tafadhali nisamehe tuishi kama mwanzo malkia au mfalme wangu.

UNAVYOMPENDA
“Mpenzi, wazuri wako wengi lakini moyo wangu ulikuteua wewe, macho yangu yalikuona wewe, furaha na tabibu wa maradhi yangu dawa yake si mwingine zaidi yako, napenda tuishi sote hadi mwisho wa dahari.

UNAVYOMTHAMINI
“Mpenzi wangu, wewe ni mwanamke au mwanaume wa thamani sana katika maisha yangu. Wewe ni sehemu ya maji matamu, yenye uwezo wa kukata kiu yangu. Wewe ni sehemu ya shamba lenye rutuba nzuri niwezayo kulima mwaka mzima. Kama ni chakula basi ni kile nikipendacho kuzidi vyakula vingine.

Happy-young-couple-in-bedUNAVYOMJALI
“Mpenzi, nipo tayari kuchangia nawe simu moja ilimradi uamini tu kuwa nakupenda na uko pekee yako moyoni mwangu. Najua kuna wakati nakukwaza kama binadamu, nisamehe, usinichukie siku zote.

NDUGU, RAFIKI
“Rafiki yangu, nilikukosea sana ila naomba msamaha wako ili urafiki wetu uendelee kudumu kama mwanzo, najua tulikwaruzana kwa sababu ya hapa na pale lakini bado sisi ni wanadamu, tumeumbiwa makosa, tusameheane.

“Najua ndugu yangu nilikukosea, nisamehe, natambua mchango wako katika maisha yangu, thamani na upendo wangu kwako vitaendelea kudumu moyoni mwangu siku zote, tudumu milele hadi kifo kitutenganishe.”

Wapenzi wasomaji wetu tunapenda kuwatakiwa Valentine’s Day njema. Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, Instagram: mimi_na_uhusiano au unaweza kujiunga kwenye group letu la WhatsApp kwa elimu zaidi ya mapenzi.

Leave A Reply