The House of Favourite Newspapers

Video: Undani meneja wa Diamond kudaiwa Mil. 250

0

babu-tale Hamis Taletale ‘Babu Tale’.

Andrew Carlos na Boniphace Ngumije, Risasi Jumamosi

BAADA ya hivi karibuni Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutoa hati ya kukamatwa kwa Meneja wa ‘Diamond Platnumz’, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ kwa kutotii amri ya kumlipa Shehe Hamis Mbonde Sh. Milioni 250, kisha yeye kuibuka na kukanusha madai hayo, kiongozi huyo wa dini naye amefunguka kwa kirefu undani wa suala hilo, Risasi Jumamosi lina mchongo kamili.

babu-taleBabu Tale na Diamond.

BABU TALE ALIMFUATA KWAKE

Gazeti hili lilifunga safari hadi kwa shehe huyo, Chamazi jijini Dar na ambako alielezea kwa kirefu sakata hilo lilivyokuwa mwanzo mwisho.

“Ishu nzima ilikuwa mwaka 2013 ambapo nikiwa hapa nyumbani kwangu (Chamazi) walikuja watu waliojitambulisha kuwa ni viongozi wa Kampuni ya Tip Top Connection, wakajitambulisha kulikuwa na Mwarabu, Abdu Bonge (marehemu), Iddi Tale, Babu Tale na Adam Mwakuhama ‘Madenge’ aliyejitambulisha kama Meneja,” alisema Mbonde.

    shehe (4) Shehe Hamis Mbonde

WAMPA AHADI KIBAO

Baada ya kujitambulisha walimwambia kilichowapeleka kuwa walikuwa wakimuomba aingie makubaliano ya kufanya naye kazi pamoja ambapo watakuwa wakifanya biashara ya kurekodi mawaidha na kutengeneza nakala za DVD kwa ajili ya kuzisambaza nchi nzima (kwenye misikiti) na kuziuza.

“Niliwakubalia kwa kuwa waliniambia kuwa wataninunulia nyumba, gari na kunipa Sh. Milioni 50 kama kianzio. Nilikubali mbele ya mashahidi wangu wawili waliokuwepo siku hiyo,” aliongeza Shehe Mbonde.

shehe (1)WAMGEUKA

Shehe Mbonde anaendelea kutiririka kuwa baada ya kukubaliana bila kulipana chochote huku akipewa miadi ya kwenda kufanyiwa ‘process’, baada ya wiki kadhaa aliitwa ofisini kwao.

“Waliniita na kuniambia kuwa tuanze kazi ya kurekodi wakati nikisubiri vile walivyoniahidi, walinipa shilingi milioni mbili na kuniambia hazipo kwenye ahadi ile kubwa, bali ni kama kifuta jasho pindi watakapokuwa wakinitumia katika kusambaza DVD.

shehe (6)Kasha la DVD hiyo.

“Nilichukua kiasi kile cha pesa na baada ya mwezi nilishangaa kusikia DVD zangu (mojawapo Uzito wa Kifo) zikiuzwa kila kona pasipo kunishirikisha kwa lolote. Nikawapigia simu, walinijibu kwamba siwadai kitu, niende popote na nifanye niwezavyo. Basi nikachukua mawakili wangu watatu (Mwesigwa Muhingo, Gwamaka Mwaikugile na Clement Kihoko) wakasimamia kesi hiyo,” alisema shehe huyo.

shehe (5)KESI YAANZA KUNGURUMA

Mawakili hao walifungua kesi ya madai namba 185/2013 wakiomba mahakama iamuru wadaiwa wamlipe Shehe Mbonde Sh.Milioni 700 kama fidia ya kukiuka makubaliano na Sh. Milioni 50 kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na kuvunjwa kwa makubaliano.

Baada ya kesi hiyo kuanza kuunguruma, watuhumiwa hao waliitwa mahakamani na Madenge alithibitisha kumjua mdai na kwamba vyote vilivyokuwa vikilalamikiwa ni kweli.

“Kesi iliendelea kuanzia 2013, Februari mwaka huu nilishinda kesi na mahakama ikamuamuru Babu Tale alipe kiasi hicho cha fedha, tukakaa kimya kuanzia mwezi huo lakini hadi Juni hakuwa ameripoti hivyo mahakama ikaamuru atafutwe.

Hivi ni baadhi ya vielelezo vya madai hayo.

shehe (2)

shehe (3)

shehe (7)

shehe (8)BABU TALE ASAKWA

“Tulienda kwa Mkuu wa Polisi Kanda ya Ilala kupata usaidizi wa kukamatwa kwa Babu Tale lakini kutokana na kuwa amehama makazi aliyokuwa amepanga (Tabata, Ilala) na kuishi Mbezi Marambamawili, Kinondoni hivyo tulisaidiwa na polisi wa Mbezi kwa Yusuf na kwenda hadi nyumbani kwake.

“Tulipofika na kujitambulisha hali ilibadilika, Babu Tale alitufungulia mbwa wapatao nane kutufukuza,” alisema shehe huyo na kusisitiza kwa kuonesha nyaraka za uthibitisho kuwa  anayemdai ni Babu Tale na si Abdu kama anavyosema meneja huyo katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Hata hivyo, shehe huyo alisisitiza kuwa lazima Babu Tale atakamatwa kwa sababu mahakama kuu imeshatoa kibali kwenda kwa Kamanda Mkuu wa Polisi Ilala na kwa kuwa amehama katika wilaya hiyo taratibu za kufuatilia kibali kingine mahakamani kwenda kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya Kinondoni anakoishi kwa sasa Babu Tale zinaendelea.

MANENO YA BABU TALE

Kwa mujibu wa Babu Tale, anasema alifungua Kampuni ya Tip Top Connection pamoja na kaka yake (Abdu Bonge) na kwamba Abdu alijikita kwenye filamu na yeye muziki, hivyo hajawahi kufanya makubaliano kama hayo, labda alifanya marehemu Abdu na shehe huyo.

TAZAMA VIDEO YA MAHOJIANO YOTE HAPA

Leave A Reply