The House of Favourite Newspapers

Vanessa afungukia bata walizokula Singita

1

VANESSA NA JUX (7) Na Hamida Hassan

Wanamuziki, Vanessa Mdee na mpenzi wake Juma Jux ‘Jux’ baada ya manenomaneno kuzagaa kuwa wameachana juzikati wapenzi hao walionekana kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti iliyopo mkoani Mara kisha kwenda kula bata kwenye hoteli ya bei mbaya ya Singita.

VANESSA NA JUX (8)Akipiga stori na safu hii juzi akiwa Serengeti, Vanessa alisema kuwa, wameamua kwenda huko kwa mapumziko ya siku nne ikiwa ni sehemu ya kufanya utalii wa ndani na wamekula bata za kutosha.

VANESSA NA JUX (6)“Ni mambo ya utalii wa ndani, tumekuja huku kupumzika kidogo, siyo lazima kwenda nchi za nje kwa mapumziko, humuhumu Bongo kuna sehemu unakwenda na unajisikia furaha,” alisema mwanadada huyo.

Singita ni hoteli ya kifahari iliyopo mkoani Mara ambayo inaiingizia nchi fedha nyingi za kigeni.VANESSA NA JUX (4)

1 Comment
  1. Halirose says

    Wow! Mmependeza jamana hadi raha yaani Mungu azidi kuwapigania daima muwe pamoja mzae watoto wengiii warembo na ma handsomeboys kama wazazi wao,

Leave A Reply