Video: Mbunge LEMA Afunguka Baada Ya Kuwa Mwenyekiti Kanda Ya Kaskazini

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Kaskazini katika uchaguzi uliofanyikaJumamosi Novemba 30, 2019 mjini Arusha.

 

Katika uchaguzi huo Lema alipata kura 78 na kumshinda mpinzani wake mbunge wa Rombo, Joseph Selasini aliyepata kura 27.

 

Wakati akijinadi Lema alieleza kuwa anawania nafasi hiyo kukitumikia chama hicho na kujiandaa kuwa mwenyekiti wa Taifa.

 

Katika uchaguzi huo  mbunge wa Viti Maalumu, Yosepher Komba alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa kanda hiyo kwa kupata kura 76 kati ya 106.


Loading...

Toa comment