The House of Favourite Newspapers

Vyakula vinavyopunguza unene

0

294D1D5C00000578-3107842-image-m-4_1433264772130Njia kuu ya kupunguza unene ni pamoja na kuchagua vyakula vya kula yaani kujua aina ya vyakula unavyotakiwa kuvila.

Vifuatavyo ni vyakula, mboga na matunda ambayo vikiliwa kwa mpangilio mzuri, huondoa mafuta ya ziada mwilini na hivyo kupunguza unene:

MATUNDA

Matunda ni miongoni mwa vyakula vinavyoyeyusha mafuta mwilini, idadi kubwa ya matunda huwa na kiwango kidogo cha ‘calories’ lakini yana kiasi kingi cha kamba lishe (fiber). Hivyo, unaweza kuchanganya ulaji wa matunda na vyakula vyenye mafuta bila kuongezeka unene. Matunda kama machungwa, zabibu, mapera ni miongoni mwa matunda yenye kiasi kingi cha kamba lishe. Tikitimaji lina uwezo wa kuondoa sumu mwilini (toxins) ambayo huingia kwa njia ya chakula na hewa tunayoivuta.

MBOGA ZA MAJANI

Mboga nyingi za majani huwa na kiasi fulani cha kamba lishe. Mbogamboga zinazochukua muda kuyeyuka tumboni lakini zinasaidia sana usagaji wa chakula haraka ni pamoja na mchicha, spinachi, kabeji, maharage ya kijani na nyingine jamii ya majani kibichi.

PROTINI

Vyakula vinavyoyeyusha mafuta haraka mwilini katika jamii ya vyakula vya protini ni vyakula vya baharini kama samaki. Ili kupata matokeo mazuri na ya haraka, pendelea kula vyakula vya baharini sambamba na mboga za majani kama vile kabichi au saladi ya mbogamboga mchanganyiko.

Vyakula vingine ni vile vitokanavyo na maziwa, ngano isiyokobolewa, wali, ambavyo wakati wa kutayarisha unatakiwa kuhakikisha vinakuwa na kiwango kidogo cha mafuta asilia bila kuongezewa ya ziada.

Leave A Reply