The House of Favourite Newspapers

Wafungwa 79 Gereza Butimba Waliosamehewa na Rais Waachiliwa

0
Baadhi ya wafungwa wakiume wa Gereza Kuu Butimba Mwanza, walionufaika na Msamaha wa Rais wakitoka katika lango la Gereza hilo tayari kwenda kuungana na familia zao. Wafungwa hao wamemshukuru Rais Magufuli kwa msamaha huo wa kihistoria.

Leo Desemba 10, wafungwa 79 wameachiwa kati ya wafungwa 190 waliopewa msamaha na Rais Dkt. John Magufuli  kwa mkoa wa Mwanza huku sababu kuu ya kuachiliwa idadi hiyo ni kwasababu wengine hawajakidhi vigezo vya kunufaika na msamaha huo.

Wafungwa wa kike Gereza Kuu Butimba – Sehemu ya Wanawake wakitoka gerezani baada ya Msamaha wa Rais alioutoa jana katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru.

 

Rais Magufuli jana alitoa msamaha kwa wafungwa 5,533.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akitoa taarifa fupi ya zoezi zima la uachiliaji wa wafungwa walionufaika na msamaha wa Rais katika mikoa mbalimbali nchini mbele ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari jijini Mwanza leo Desemba 10, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo akizungumza na Wafungwa wa Gereza Kuu Butimba kabla ya zoezi la uachiliaji wa wafungwa walionufaika na Msamaha wa Rais leo Desemba 10, 2019. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Mwanza pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike wakishuhudia wafungwa walionufaika na Msamaha wa Rais katika Gereza Kuu Butimba wakipewa mali zao na nauli ya kwenda kuungana na familia zao leo Desemba 10, 2019 kabla ya zoezi la uachiliaji wa wafungwa husika wa msamaha huo.

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike (wa pili toka kulia) akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela(vazi la kitenge) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa mwanza alipowasili gereza Butimba kushuhudia zoezi la uachiliaji wafungwa walionufaika na msamaha wa Rais.
Mfungwa mnufaika wa Msamaha wa Rais, William Dingu akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) baada ya kuachiliwa huru leo. Mfungwa huyo amemshukru Rais kwa msamha huo, aidha, amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kumwezesha ujuzi wa wa fani ya ujenzi ambao ameupatia gerezani kupitia programu ya Urekebishaji inayosimamiwa na Jeshi hilo

Wafungwa 79 wa Gereza Kuu Butimba walionufaika na msamaha wa Rais waachiliwa leo Desemba 12, 2019 Jijini Mwanza.

Leave A Reply