Wakongwe wa Muziki ‘Waikalisha’ Dar Live
Abby Skills akiwakumbushia mashabiki wimbo wa Maria.
Dully Sykes akiwapagawisha mashabiki.
Juma Nature akigonga ‘nyundo’ zake.
Mabaga Fresh nao wakiwakumbusha mashabiki ‘wakati huo’.
Soggy akiimba na kuserebuka.
Shabiki akiwa amevamia jukwaa kumtunza Dully.
Soggy akiendeleza libeneke.
Juma Nature akikamua na Inspekta Haruni.
Inspekta akiendeleza burudani.
Suma G akionyesha kipaji chake cha kuimba.
ONYESHO la wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao waliwahi kutamba enzi zao, usiku wa kuamkia leo walitoa burudani kali katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live huko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam, ambapo mashabiki walionjeshwa tena utamu ulioanzisha muziki wa vijana nchini.
Moto wa furaha uliwaka katika onyesho hilo baada ya mashabiki kukumbushiwa enzi ambazo muziki huo uliibuka hapa Bongo. Baadhi ya wanamuziki ambao walitoa burudani ni Abby Skills, Juma Nature, Dully Sykes, Soggy Dog, Mabaga Fresh, Manzese Crew, Suma G, Zin Zag Crew, Solid Ground Family na Rama Mluguru.
(NA ISSA MNALLY)