The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi Laki 7 Wachaguliwa Kujiunga Form One

0

WANAFUNZI 701, 038 sawa na asilimia 92.2 waliomaliza darasa la saba wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule za serikali kwa mwaka 2020.

 

Hata hivyo, wanafunzi 58,699 sawa na asilimia 7.73 waliofaulu hawakuchaguliwa kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.

 

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ametangaza hilo leo ambapo amesema Mikoa 13 ya Geita Morogoro, Dodoma, Njombe, Katavi, Singida, Ruvuma, Tabora, Kilimanjaro, Kagera, Mwanza, Shinyanga na Mtwara wanafunzi wote wamefaulu kujiunga kidato cha kwanza 2020 kwenye Shule za Sekondari za Serikali.

 

Ikumbukwe Oktoba 15, 2019 Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) lilitangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 ambapo asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 walifaulu huku watahiniwa 909 wakifutiwa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.

Leave A Reply