Wanafunzi wa Shule ya Sekondaari ya St. Joseph’s Cathedral mapema leo wamesherehekea hafla fupi ijulikanayo kama Family Day ambayo imefanyika katika Hosteli zao zilizopo maeneo ya Don Bosco Osyter Bay jijin i Dar es Salaam.
Akizungumza na Global Tv Online mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Debora Sando alisema kuwa ni mkakati wao wa shule kila mwaka kukutana kwa pamoja kabla ya kufunga shule kuwa na siku maalum ya kufurahia ikiwa ni pamoja na kucheza michezo kama vile kuimba nyimbo, kuigiza na mambo mbalimbali.
Wanafunzi hao kabla ya kuanza kwa hafla hiyo walianza kwa ibada maalum ambayo pia ilihusisha Mkuu wa Shule ya St. Joseph Cathedral, Sista Theodora Faustine ambaye alikuwa sambamba na wanafunzi hao kuhakikisha mambo yote yanaenda sawa.