The House of Favourite Newspapers

Wasifu wa Kocha Mpya wa Simba, Sven Vandenbroeck

0

JANA Desemba 11 Mabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara Simba Sports Club wamemtangaza Kocha Mkuu wao mpya Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck. Hatua hiyo inafuatia Simba kuvunja mkataba wake na Mbelgiji mwingine Patric Aussems (Uchebe).

 

Hapa chini ni wasifu (CV) ya kocha huyo mpya wa Simba.

Sven alizaliwa Septemba 22 mwaka 1979 nchini Ubelgiji katika mji wa Vilvoorde, ikiwa na maana kwamba anajiunga na Wekunde wa Msimbazi akiwa na umri wa miaka 40.

 

Kati ya mwaka 1996 hadi mwaka 2009, alikuwa mchezaji wa soka katika vilabu tofauti 6 kwanza nyumbani kwao Ubelgiji, kisha Uholanzi, Ugiriki na Norway.

 

Mwaka 2014 akaanza rasmi kazi yake ya ukufunzi wa soka akianza na Klabu ya Niki Volos ambayo sasa inashiriki Ligi Daraja la Tatu nchini Ugiriki.

 

Mwaka 2017 Sven alikuwa Kocha Msaidizi wa Kocha Hugo Broos wakati alipoiongoza Timu ya Taifa ya Sok ya Cameroon kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika.

 

Mwezi Julai mwaka 2018 Sven akatangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zambia maarufu kama Wanachipolopolo au The Copper Bullets, moja ya kazi zake ikawa kuhakikisha timu hiyo inafuzu kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika Mwaka 2019.

 

Machi 2019 Shirikisho la Soka Zambia likamtimua kazi kwa kushindwa kuifanya Timu ya Taifa hilo kufuzu Kombe la Mataifa Afrika.

 

Leo Disemba 11 2019, Wekunde wa Msimbazi wamemtangaza Sven kuwa kocha Mkuu mpya wa Timu hiyo na wanaamini ndiye mwalimu sahihi kufundisha mabingwa hao na kusonga mbele zaidi.

 

Leave A Reply